China yawatenganisha watoto wa Kiislam na familia zao kudhibiti imani ya kidini

Hotan Sunshine Kindergarten
Image caption Muonekano wa kituo cha Hotan kupitia uzio wa waya

China imekuwa ikiwatenganisha kimakusudi watoto wa Kiislamu na familia zao, dini na lugha yao katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa utafiti mpya.

Mamia ya watu pia wanazuiliwa katika kambi kubwa huku mpango wa kujenga shule ya bweni ukiendelea.

Kulingana na stakabadhi za umma zilizofuatiwa na mahojiano kadhaa ya familia zinazoishi ughaibuni BBC, imepata ushahidi mkubwa kufikia sasa kuhusu kile kinachofanyiwa watoto katika eneo hilo.

Rekodi zinaonesha kuwa watoto 400 wametenganishwa na wazazi wao iwe ni kufungiwa katika kambi au jela.

Ukaguzi unafanywa kubaini ikiwa watoto hao wanahitaji ''uangalizi maalum".

Image caption Shule ya chekechea ya Hotan sawa na zingine hupewa ulinzi

Kutokana na udhibiti mkali wa salama wa eneo la Xinjiang,wanahabari wa kimataifa wanafuatiliwa saa 24 hali ambayo inakuwa vigumu kusema na wahasiriwa.

Lakini baadahi yao wanapatikana nchini Uturuki.

Katika ukumbi mmoja mkubwa mjini Istanbul, makumi ya watu wanapanga foleni wakiwa wameshikilia picha za watoto wao zinazosimulia jinsi walivotoweka nyumbani.

"Sijui ni nani anawatunza," mama mmoja alisema huku akionesha picha ya binti zake watatu wadogo, "hauuna mawasiliano kabisa."

Mama mwingine aliyekuwa ameshikilia picha ya watoto wake watatu wa kike na mmoja wa kiume analia akisema: "INasikia kuwa wamepelekwa katika kituo cha kulea watoto,"

Katika mahosjiano 54 tofauti wazazi wamesimulia jinsi watoto wao zaidi ya 90 walivyopotea Xinjiang.

Wote ni wanatokea jamii ya Uighurs - na wengi wao ni waumini wa dini ya kiislamu ambao wamekuwa na ushirikiano mkubwa wa kidini na taifa la Uturki

Maelfu yao wako nchini humo kwa masomo, kufanya biashara, kutembelea familia zao au wametoroka sera ya Uchina ya uzazi wa mpango na ukandamizaji wa kidini.

Lakini miaka mitatu iliyopita wamejikuta mashakani baada ya China kuanza kuwakamata mamia ya watu wa jamii ya Uighur na kuwazuilia katika kambi maalum.

Mamlaka za China zinasema kuwa watu wa jamii ya Uighurs wanapewa elimu katika "vyuo vya kiufundis" ili kukabiliana na itikadi kali za kidini.

Lakini ushahidi unaonesha kuwa wengi wao wanafungiwa katika vituo hivyo ili kuwazuia kufuata muongozo wao wa kidini kama vile kusali na kuvaa nguo zinazoashiria misimamo yao ya kidini au kuwazuia kusafiri mahali kama Uturuki.

Kutokana na hali hizo kwa watu wa Uighurs, kurudi nyumbani kunamaanisha kwenda kuzuiliwa katika vituo hivyo.

Nambari zao za simu zimenakiliwa - kumaanisha hata kuzungumza na jamaa wako aliye nje ya nchi ni hatari katika mji wa Xinjiang.

Mtu mmoja ambaye mke wake amefungiwa aliiambia BBC kuwa anahofia huenda watoto wake wanane wako mikononi mwa serikali.

"Nadhani wanasomeshwa katika vituo hivyo" alisema.

Utafiti mpya uliofadhiliwa na BBC unaangazia kile wanachofanyiwa watoto hao na maelfu ya wengine.

Dr Adrian Zenz ni mtafiti wa Ujerumani ambaye alisifika sana kwa kufichua jinsi China imekuwa ikiwazuilia waumini wa dini ya Kiislamu mjni Xinjiang.

Kulingana na maelezo yalio wazi kwa umma na ripoti yake inaashiria kuna mpango wa kupanua shule katika eneo la Xinjiang.

Jimbo hilo limekua likiimarisha juhudi zake ili kukidhi mahitaji ya idadi kubwa ya watoto wanaozidi kuongezeka.

Katika kipindi cha mwaka mmoja idadi ya watoto wanaojiunga na shule za chekechea katika Jimbo la Xinjiang imeongezeka kwa zaidi ya nusu milioni.

Watoto kutoka jamii ya Uighur na waislamu wengine wanakadiria 90% ya ongezeko hilo.

Kutokana na hilo kiwango cha watoto wanaojiunga na shule hizo imeongezeka na kupita kiwango kilichowekwa na serikali.

Katika eneo la Kusini mwa Xinjiang, amabko kuna idadi kubwa ya watu wa Uighur, mamalaka imejenga vituo vipya vya watoto kwa thamani ya dola bilioni $1.2.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii