NEC imekiuka sheria kutangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Singida Mashariki?
Huwezi kusikiliza tena

NEC imekiuka sheria kutangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Singida Mashariki?

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza tarehe 31 Julai, 2019, kuwa siku ya kufanyika uchaguzi mdogo Jimbo la Singida Mashariki lililokuwa likishikiliwa na Tundu Lissu ambaye kwa sasa yuko nchini Ubelgiji kwa matibabu baada ya Spika Job Ndugai kutangaza kuwa jimbo hilo liko wazi.

Akitangaza hatua hiyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage, amesema ratiba inatokana na barua ya spika inayoeleza kuwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Tundu Lissu amepoteza sifa ya kuwa Mbunge kutokana na kushindwa kuwasilisha kwa spika tamko la mali na madeni na kushindwa kuhudhuria mikutano saba mfululizo bila ruhusa ya Spika.

"Tumezingatia matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, kutoa taarifa kwa umma kuhusu uwepo wa uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki," alisema Jaji Semistocles Kaijage.

Ameelezea pia kwamba fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya Julai 13 hadi 18 mwaka huu, ambapo uteuzi wa wagombea utafanyika Julai 18, na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia Julai 19 hadi 30 na siku ya uchaguzi itakuwa ni Julai 31, mwaka huu.

Je, sheria inasema nini kuhusu Tume ya uchaguzi kutangaza uchaguzi mdogo?

Mwandishi wa BBC Scolar Kisanga amezungumza na Mwanasheria Anna Henga

Mada zinazohusiana