Mpiga mbizi aifichua siri ya firauni katika makaburi ya chini ya maji Sudan

Figurine Haki miliki ya picha Nuri Archaeological Expedition/ PearcePaulCreasman

Mwanaakiolojia wa kupiga mbizi ameieleza BBC kuhusu jitiahada aliyopitia kulifikia kaburi la firauni chini ya piramidi.

Pearce Paul Creasman na kikosi chake ni watu wa kwanza kuingia katika kaburi hilo katika mipindi cha miaka 100 na katika muda huo, imekuwa vigumu kulifikia kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha maji baharini.

Creasman ameiambia BBC kwamba ni mara ya kwanza uchimbaji wa chini maji unafanyika katika akiolojia nchini Sudan, eneo la jadi alikozikwa Nuri.

Aligundua vitu vilivyotengenezwa kwa udongo na dhahabu iliyopondwa.

Haki miliki ya picha Nuri Archaeological Expedition/PearcePaulCreasman

"Dhahabu hiyo ilikuwa ingalipo - sanamu hawa wadogo wa vigae walikuwa wamefunikwa kwa dhahabu. Na wakati maji yaliiharibu vigae vilivyokuwa chini, chembe chembe za dhahabu bado zilikuwepo," ameeleza.

Anaamini zawadi hizo zilikuwa ni za Nastasen, firauni mdogo alioyetawala ufalme wa Kush kingdom tangu 335 BC hadi 315 BC.

Dhahabu hii huenda ingelichukuliwa na wezi lau kama hakunge kuwepo na kiwango kikubwa cha maji yanayozuia kufikiwa kaburi hilo, mwanaakiolojia wa chini ya maji Kristin Romey ameandika katika National Geographic.

Creasman ameiambia BBC kwamba kikosi hicho "kilichimba chini kadri ya uwezo wao" chini ya ngazi yenye vidaraja 65 iliolekea katika mlango wa liliko kaburi hilo lakini "tulishuka hadi katika daraja la 40 mpaka tulipofika chini sakafuni na tukatambua hatuwezi kushuka tena pasi kuzamisha vichwa".

Haki miliki ya picha Nuri Archaeological Expedition / Arthur Piccinati

Walitumia bomba iliyotoa hewa ya oxygen kutoka juu ardhini wakati walipopiga mbizi mwezi Januari.

Ameeleza kwamba walistaajabishwa kwa walichokigundua:

"Kuna sehemu tatu, zilizo na sehemu ya juu iliyo chongwa zenye ukubwa wa basi dogo la usafiri unaingia katika sehemu moja na kutokea katika nyingine ni giza, unajua uko ndani ya kaburi, iwapo hukuwasha tochi.

Na siri ya yaliomo ndani zinaanza kufichuka."

Taarifa nyingine ambazo huenda zikakuvutia:

Kaburi hilo ni sehemu ya maenoe ya jadi ya Nuri yalioenea katika ardhi yenye ukubwa zaidi ya ekari 170 kaskazini mwa Sudan.

Piramidi zinaonyesha maenoe walikozikwa wafalme wa Kushite ambao mara nyingine huitwa "firauni weusi". Ufalme wa Kush ulikuwepo kwa miaka mia kadhaa na katika karne ya 8 BC uliitawala Misri ambayo iliiongoza kwa takriban karne moja.

Haki miliki ya picha Nuri Archaeological Expediton/PearcePaulCreasman

Tofauti moja kati ya piramidi zilizopo Sudan na zile maarufu zilizopo nchini Misri ni kwamba wafalme walizikwa chini ya piramidi hizo badala ya ndani yake.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii