Kwa nini wanawake walio katika hedhi nchini India wanatoa mifuko yao ya uzazi?

Unyanyapaa wa hedhi nchini India Haki miliki ya picha AFP
Image caption Unyanyapaa wa hedhi nchini India

Taarifa mbili za habari za kusikitisha zinazowahusu wanawake na hedhi zimetangazwa nchini India katika miezi ya hivi karibuni.

Hedhi imekuwa mwiko katika taifa hilo, na wanawake walio katika hedhi wanadaiwa kutokuwa wasafi na hutengewa katika mihadhara ya kijamii na ile ya kidini.

Katika miaka kadhaa, mawazo hayo yamepigwa vita hususan na wanawake wasomi wanaoishi mijini.

Lakini ripoti mbili za hivi karibuni zinaonyesha kuwa uhusiano wenye utata kati ya hedhi na taifa hilo unaendelea.

Wanawake wengi hususan wale wanaotoka katika familia masikini wasio na elimu hulazimika kuchagua hatua ambazo huathiri afya na maisha yao kwa muda mrefu.

Habari ya kwanza inatoka kutoka jimbo la magharibi la Maharashtra ambapo imebainika na vyombo vya habari vya India kwamba maelfu ya wasichana hufanyiwa upasuaji kuondoa vizazi vyao katika kipindi cha miaka mitatu iliopita .

Wengi wao wamechukua hatua hiyo ili kupata kazi ya kuvuna miwa.

Kila mwaka , makumi ya maelfu ya wanawake kutoka familia masikini kutoka Beed, Osmanabad, Sangli na wilaya ya Solapur husafiri kuelekea wilaya zilizoendelea za jimbo hilo zinazojulikana kama ukanda wa sukari ili kufanya kazi kwa miezi sita kama wakataji miwa katoka mashamba ya miwa.

Wakati wanapokuwa huko , wako chini ya wanakandarasi wenye tamaa wanaowatumia vibaya.

Mwanzo, hukataa kuwaajiri wanawake kwa kuwa ukataji wa miwa ni kazi ngumu mbali na kwamba wanawake huweza kukosa siku moja ama mbili kutokana na hedhi.

Iwapo wanakosa siku moja hulazimika kulipa faini.

Mazingira ya kufanyia kazi sio mazuri hivyobasi familia hizo hulazimika kuishi katika mahema ama vibanda karibu na mashamba , hakuna vyoo na kwa sababu uvunaji miwa mara nyengine hufanyika hadi nyakati za usiku hakuna muda uliowekwa wa kulala ama kuamka.

Na wakati wanawake wanapokuwa katika hedhi -hukumbwa na hali ngumu sana.

Kutokana na hali mbaya ya usafi , wanawake wengi hupata maambukizi kulingana na wanaharakati wanaofanya kazi katika eneo hilo hivyobasi madaktari wasio na maadili huwashinikiza kufanyiwa upasuaji hata wanapotembelea hospitali kwa matatizo madogo ya uzazi ambayo yanaweza kutibiwa kwa kumeza dawa.

Na kwa kuwa wanawake wengi katika eneo hili wameolewa wakiwa wachanga , wengi wao hupata watoto wawili ama hata watatu wakati wanapokuwa katika umri wa miaka 20 na kwa sababu madaktari hawawaambii kuhusu matatizo yanayowakumba wakati wanapofanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi chao , wengi huamini kwamba ni sawakufanyiwa hivyo.

Hatua hii imefanya vijiji vingi katika eneo hilo kuwa na wanawake wasio na vizazi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya wanawake nchini India hufanya kazi kama wavunaji miwa

Baada ya swala hilo kuwasilishwa mwezi uliopita katika bunge la jimbo hilo na mbunge kwa jina Neelam Gorhe , waziri wa afya katika jimbo hilo la Mahashatra Eknath Shinde alikiri kwamba kumekuwa na visa 4605 vya upasuaji wa kuondoa vizazi miongoni mwa wanawake katika wilaya ya Beed ndani ya kipindi cha miaka mitatau.

lLkini alisema, sio wanawake wote wanaofanya kazi katika Miwa walifanyiwa upasuaji huo.

Waziri huyo alisema kuwa kamati imebuniwa ili kuchunguza visa kadhaa.

Mwenzangu Prajakta Dhulap kutoka huduma ya lugha ya BBC ya Marathi ambaye alitembelea kijiji cha Vanjarwadi wilayani Beed anasema kuanzia mwezi Oktoba hadi Machi kila mwaka asilimia 80 ya wanavijiji husafiri kwenda kufanya kazi katika mashamba ya miwa .

Ameripoti kwamba nusu ya wanawake katika kijiji hivyo wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa vizazi vyao - wengi wao wakiwa chini ya miaka 40 huku wengine bado wakisalia chini ya umri wa miaka 40 huku wengine wakiwa katika miaka ya 20.

Wanawake wengi aliokutana nao walisema kuwa hali yao ya afya imedorora tangu walipofanyiwa upasuaji huo.

Mwanamke mmoja alizungumzia kuhusu maumivu yasiokwisha katika mgongo wake , shingo na magoti na vile anavyoamka alfajiri akiwa na mikono yenye vidonda , uso na miguu.

Mwengine alilalamikia tatizo la kuhisi kizunzi mara kwa mara na vile alivyoshindwa kutembea hata eneo lisilo umbali.

Wengi wao wanasema kwamba hawawezi tena kufanya kazi katika mashamba hayo..

Habari ya pili ya kusikitisha kutoka kusini mwa jimbo la Tamil Nadu , pia ni mbaya. Wanawake wanaofanya kazi katika kampuni za kushona nguo wanadai kwamba wamepatiwa dawa zisizo na majina kazini badala ya kuruhusiwa kwenda nyumbani wanapohisi uchungu wa hedhi.

Kulingana na wakfu wa Thomson Reuters, uliowahoji wanawake 100 , dawa hizo hazikuwa zilkitolewa mara kwa mara na madaktari na washonaji hao wanaotoka katika familia masikini wanasema kuwa hawawezi kukosa mshahara wa siku moja kutokana na uchungu wa hedhi.

Wanawake wote 100 ambao walihojiwa wanasema kuwa walipokea dawa na zaidi ya nusu ya idadi yao wanasema kuwa afya yao imedorora.

Wengi wanasema kuwa hawakutajiwa jina la dawa hiyo ama hata kuonywa kuhusu madhara yake.

Wanawake wengi wamelaumu dawa hizo kwa kuwasababishia matatizo ya kiafya kutokana msongo wa mawazo, maambukizi ya njia ya mkojo na kutokwa kwa mimba.

Ripoti hiyo imelazimu utawala wa eneo hilo kuchukua hatua. Tume ya kitaifa ya wanawake imetaja hali hiyo ya wanawake wa Maharashtra kuwa mbaya na kulitaka jimbo hilo kuzuia ukatili huo katika siku za usoni.

Katika jimbo la Tamil Nadu serikali imesema kuwa itachunguza afya ya wafanyikazi hao wa kushona nguo.

Haki miliki ya picha Piyush Nagpal

Nchini Indonesia, Japan, Korea kusini na mataifa mengine machache - wanawake huruhusiwa kupumzika kwa siku moja wakati wakiwa na hedhi .

Kampuni nyingi za kibinafsi pia hutoa ruhusa kama hizo.

Nchini India katika jimbo la Bihar limekua likiwaruhusu wanawake kuchukua siku mbili za ziada kila mwezi.

Na mwaka uliopita mbunge mmoja wa kike aliwasilisha muswada wa faida za hedhi bungeni akitaka wanawake kupewa siku mbili kila mwezi kwa kila mwanamke anayefanya kazi nchini humo.