Marekani haipaswi 'kukaa kimya' kuhusu kifo cha Khashoggi mjini Instabul

Vizuizi vya kiulinzi nje ya ubalozi wa Saudia mjini Istanbul Haki miliki ya picha Reuters

Marekani inapaswa kuchukua hatua kuhusu ripoti ya uchunguzi kuhusu kifo cha mwanahabari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi kilichotokea mwezi Oktoba mwaka jana, afisa wa shirika la umoja wa mataifa ameeleza.

''Hawawezi kuchagua kunyamaza, wanapaswa kuzungumza, lakini haitoshi. Tunapaswa kuchukua hatua'', amesema Agnes Callamard.

Uchunguzi ulihitimisha kuwa kifo cha Khashoggi kwenye ubalozi wa Saudi Arabia mjini Instanbul ''ilikuwa ni mauaji ya kinyama''.

Akizungumza akiwa pembeni mwa mchumba wa Khashoggi, bi Callamard ameitaka Marekani kukiri kutowajibika ipasavyo katika kuchukua hatua

Ripoti ya bi Callamard ya kurasa 101, iliyochapishwa mwezi Juni, imesema kulikuwa na ''ushahidi wa kuaminika'' kuwa mwana mfalme Mohammed bin Salman na maafisa wengine wa juu wanawajibika kwa mauaji ya Jamal Khashoggi.

Vyombo vya usalama vya Saudia vilimuua mwandishi wa habari ndani ya ubalozi wa Saudia mjini Instabul lakini mamlaka zinasisitiza walikuwa they were not acting on Prince Mohammed's orders.

Bi Callamard ametoa wito kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuanzisha uchunguzi wa tukio hilo, lakini alisema nchi mwanachama pekee ina mamlaka ya kufanya hivyo.

Amesema nchi za magharibi haziwajibiki kwa kusikiliza vilio vya watu kuhusu mauaji.

Hiki ndicho kikosi 'kilichomuua' Khashoggi

Saudi Arabia kuwachunguza wahusika wa mauaji ya Khashoggi

Mchumba wa marehemu Khashoggi, Hatice Cengiz ametoa wito kwa nchi za Ulaya ''kuitilia maanani zaidi ripoti hii''.

''Ni hatari sana kufanya kama hakuna kilichotokea,'' alisema.

Je Jamal Khashoggi aliuawa vipi?

Mwandishi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 59 , na aliyekuwa akiandikia gazeti la the Washington Post na mkosoaji mkubwa wa mwanamfalme Mohammed mara ya mwisho alionekana akiingia katika ubalozi wa Saudia tarehe 2 Oktoba ili kuchukua nakala alizohitaji ili kumuoa mchumba wake Hatice Cengiz.

Bi Callamard , mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kiholela alisema kuwa Khashoggi aliuawa kikatili ndani ya ubalozi huo.

Naibu wa mwendesha mashtaka wa Saudia Shalaan Shalaan aliambia maripota kwamba mnamo mwezi Novemba kwamba mauaji hayo yaliagizwa na kiongozi wa wapatanishi aliyetumwa mjini Instanbul na naibu afisa mkuu wa ujaususi ili kumlazimisha Khashoggi kurudi katika ufalme huo kutoka mafichoni kwake.

Wachunguzi waliamua kwamba Khashoggi alilshikwa kwa nguvu baada ya kukataa na kudungwa sindano iliokuwa na kiwango cha juu cha dawa hatua iliosababisha kifo chake'', alisema bi Shaalan .

''Mwili wake baadaye ulikatwakatwa na kupatiwa mshirika wa ajenti hao nje ya ubalozi'', aliongezea.

Watu watano tayari wamekiri kumuua, bi Shaalan alisema akiongezea '' mwanamfalme hakuwa na habari kuhusu hatua hiyo''.

Ripoti inasemaje ?

Mnamo mwezi Januari afisi ya haki za kibinaadamu katika Umoja wa Mataifa ulimpatia bi Callamard jukumu la kuchunguza kuhusu kiwango cha utaifa na watu binafsi waliohusika katika mauaji hayo.

Maafisa waandamizi wa Saudia wanasisitiza kuwa kifo cha Khashoggi kilitokana na operesheni mbaya , lakini mchunguzi huyo wa UN anasisitiza kuwa ni mauaji ya kiholela ambapo ufalme wa Saudia unadaiwa kuhusika.

Haki miliki ya picha Reuters

Kutokana na sheria ya haki za kibinaadamu, jukumu la serikali sio swali kwa mfano, ni maafisa gani wa serikali waliagiza mauaji ya Khashoggi, iwe mmoja ama zaidi aliagiza kutekwa kwake kabla ya kudaiwa kuwa ajali ama iwapo maafisa hao walitekeleza mauaji hayo kibinafsi.

Bi Callamard pia alisema kuwa kulikuwa na ushahidi uliotaka uchunguzi zaidi kufanywa kuhusu maafisa wa ngazi za juu.

Mtaalamu huyo anasema kwamba mwanamfalme huyo anahitaji kuwekewa vikwazo ambavyo tayari vinaaathiri mataifa wanachama ikiwemo Marekani, dhidi ya watu binafsi waliotajwa kuhusika na mauaji hayo.

Amesema kuwa vikwazo hivyo vinafaa kulenga mali yake katika mataifa ya kigeni, hadi pale ushahidi utapatikana kwamba hakuhusika na mauaji ya bwana Khashoggi", alisema.

Kesi ya washukiaw hao 11 inayoendelea nchini Saudia inafaa kusitishwa kulingana na Callamard , kwa kuwa huo ulikuwa uhalifu wa kimataifa ambapo inaweza kuendeshwa mahala popote.

Hatua hiyo itaruhusu mataifa kama vile Uturuki , Marekani kuweza kuwashtaki wauaji wake.

Ripoti hiyo inasema kuwa baraza la Umoja wa Mataifa linafaa kufuatilia uchunguzi kuhusu mauaji ya Khashoggi ili kuanzisha kesi kubwa na kutafuta mikakati kwa watu kuchukua jukumu kama vile jopo.

Hakujakuwa na tamko lolote kuhusu ripoti hiyo kutoka kwa serikali ya Saudia.