Ole Gunnar Solskjaer: Kuna 'ajenda' dhidi ya Paul Pogba

Paul Pogba Haki miliki ya picha Getty Images

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa Paul Pogba ''hajawahi kuwa tatizo'' na kuwa kuna ''ajenda'' dhidi ya kiungo huyo mfaransa.

Wakala wa Pogba, Mino Riola amesema mchezaji huyo, 26, anataka kuondoka united na ana matumaini kuwa ''kutakuwa na suluhu lenye kuridhisha kwa pande zote''.

Pogba alisema mwezi Juni kuwa ''sasa inaweza kuwa muda mzuri wa kuhamia sehemu nyingine''.

Solskjaer amesema klabu haijapokea maombi ya usajili kwa mchezaji yeyote.

''Ni ajenda dhidi ya Paul, ni mchezaji mzuri, mzuri sana, hakujawahi kuwa na shida, ana moyo wa dhahabu,'' alisema kocha huyo.

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 10.07.2019

"Pogba hana kosa lolote"

''Paul hakuwahi kujiweka nje ya timu, mara zote amekuwa akitoa mchango wake mzuri na siwezi kuripoti chochote , isipokuwa maneni ya mawakala ya wakati wote.

''Siwezi kukaa hapa kumzungumzia Paul na kila wanachokisema mawakala, tuna miaka michache iliyobaki kwenye mkataba wake na ni mchezaji mzuri.''

'Sisi ni Man United'

United wamemsajili winga Daniel James kutoka Swansea na mchezaji wa timu ya taifa ya England anayechezea kikosi cha umri wa chini ya miaka Aaron Wan -Bissaka wa Crystal Palace kwa kitita cha pauni milioni 50.

''Sisi ni Manchester United, hatuna na haja ya kuuza wala kutoa pesa maradufu. Unapaswa kuwa na wachezaji sahihi kwa bei sahihi na ukikitazama kikosi tulichonacho sasa, kuna wachezaji wazuri wengi.

Mada zinazohusiana