Balozi wa Uingereza nchini Marekani ajiuzulu baada ya kuukosoa utawala wa Trump

Sir Kim Darroch Haki miliki ya picha PA Media

Balozi Kim Darroch anayewakilisha Uingereza nchini Marekani, amejiuzulu yakiwa ni matokeo ya kuvuja kwa barua pepe zinazoukosoa utawala wa rais wa Marekani, Donald Trump.

Balozi huyo, aliitwa ''mtu mpumbavu'' na rais Trump, baada ya barua pepe hizo kusema utawala wa Trump si stadi''.

Ofisi ya mambo ya nje imesifu hatua ya Balozi Kim ''kwa weledi wake''.

Balozi huyo amesema anataka kumaliza mzozo uliokuwepo, na kuongeza kuwa kuvuja kwa barua pepe kumefanya utenda kazi wake kuwa ''mgumu''.

Katika barua yake kwa wizara ya mambo ya nje Kim alisema: '' tangu kuvuja kwa nyaraka za kiofisi kutoka ubalozi huu kumekuwa na hisia kuhusu nafasi yangu na muda wangu uliobaki kama balozi.

Marekani na Uingereza zarushiana cheche za maneno - kunani?

Uchunguzi wa Barua pepe zilizovuja dhidi ya utawala wa Trump waanza

''Ninataka nizimalize hisia hizo.''

Akijibu barua hiyo Simon McDonald, mkuu wa masuala ya diplomasia, amesema balozi Kim ametumikia majukumu yake vyema, kwa ustadi na heshima''.

Akieleza kuwa kuvuja kwa barua pepe ni tukio la ''hila'' aliongeza Simon: ''Wewe ni bora kwetu.''

Theresa May alisema ilikuwa ''suala la kujutia sana'' kuwa bwana Darroch amejisikia kuwa anahitaji kuachia ngazi, akisema maafisa wanapaswa kuwa na uwezo wa kutoa ''ushauri wa kweli''.

''Kim alijitolea kufanya kazi kutumikia Uingereza na tuna deni la shukrani kwake,'' aliongeza

Waziri Mkuu amesema Baraza lote la mawaziri lilikuwa likimuunga mkono wakati wote wa mzozo.

Kiongozi wa chama cha Labour, Corbyn aliliambia bunge : ''Kauli zilizotolewa kuhusu yeye si za haki na si sawa. Ninafikiri amefanya utumishi mwema na anapaswa kushukuriwa.''

Balozi Kim alikuwa anatarajiwa kuondoka kwenye nafasi hiyo mwishoni mwa mwaka.

Je Sir Kim Darroch ni nani?

Sir Kim anawakilisha malkia wa Uingereza na serikali ya Uingereza nchini marekani.

Akiwa mzaliwa wa Kusini mwa Stanley , County Durham mwaka 1954 alisomea chuo kikuu cha Durham University ambapo alisomea elimu ya wanyama.

Wakati wa kipindi chake cha miaka 42 kama mwanadiplomasia amekuwa mtaalam wa usalama wa kitaifa na serza muungano wa Ulaya. Mwaka 2007 , bwana Sir Kim alihudumu Brussels kama katibu a kudumu wa Uingereza katika muungano wa Ulaya.

Alikuwa balozi wa Uingereza nchini marekani miezi kadhaa kabla ya rais donald trump kuwa rais.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii