Mahakama: Trump kuwazuia wanaomkosoa ni 'kinyume cha katiba'

@realDonaldTrump ina zaidi ya wafuasi milioni 60 Haki miliki ya picha Twitter

Rais wa Marekani Donald Trump anakiuka sheria ya kutoa maoni kwa uhuru kwa kuwafungia wanaomkosoa kwenye ukurasa wake wa Twitter, mahakama ya New York imeeleza.

Hukumu hiyo imekuja baada ya kesi iliyofunguliwa kwa niaba ya watu saba ambao walifungiwa na Trump kuingia kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Maafisa wanaotumia mitandao ya kijamii walikuwa hawaruhusiwi kuwanyamazisha watu wanaowapinga kwenye mtandao.

Mawakili wa Trump wamesema kwamba akaunti ya Twitter ni yake binafsi hivyo sheria hiyo haina athari kwake.

Balozi wa Uingereza nchini Marekani ajiuzulu

Mwana wa Trump akumbwa na kihoja Chicago

Afisa wa wizara ya sheria ya Marekani imesema imesikitishwa na uamuzi uliotolewa na mahakama.

Katika hukumu yake, mahakama imesema: ''Sheria hairuhusu afisa wa Umma anayetumia mitandao ya kijamii kumzuia mtu kuingia kwenye ukurasa wa afisa kwa sababu ametoa maoni yasiyompendeza au aiyokubaliana nayo.''

Kesi moja iliwahi kufunguliwa huko Virginia na raia ambaye baadae alishinda kesi hiyo, Brian Davison ambaye alifungiwa kuingia kwenye ukurasa wa Facebook wa kiongozi wa Umma.

Haki miliki ya picha Reuters

Mjadala wa wazi

Kesi dhidi ya raisi Trump ilifunguliwa na taasisi ya Knight First Amendment Institute.

Mkurugenzi wake Jameel Jaffer alisema: kurasa za mitandao ya kijamii ya ''maafisa wa Umma ''ni majukwaa muhimu kwa ajili ya kujadili sera za serikali.

''Uamuzi huu utahakikisha kuwa watu hawaondolewi kwenye majukwaa haya kwa sababu tu ya maoni yao yenye kumkosoa kiongozi.''

Kwa mujibu wa taasisi hiyo, watu 75 wamefunguliwa tena.

Lakini 30, wakiwemo mwandishi wa vitabu Stephen King na mwanamitindo Chrissy Teigen, wameendelea kufungiwa