Kwanini matumizi ya maziwa na Ngamia yanaongezeka duniani?

CAMELS Haki miliki ya picha QCAMEL

Maziwa ya ngamia yametumika na binaadamu kwa zaidi ya miaka 6000, na mahitaji yake yanaonekana kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni duniani licha ya gharama yake kubwa.

Mara nyingi maziwa ya ngamia hutumiwa na jamii za wafugaji na wahamiaji katika ukanda wa Afrika mashariki na pembezoni.

Jamii za Wasomali, WaBorana WaRendile na hata WaTurkana zinazopatikana katika maeneo hayo hutumia pakubwa maziwa ya ngamia kutokana na faida kama vile kusafisha mwili na kushinikiza afya ya watoto wanapokuwa.

Kadhalika kuna baadhi ambao wanaamini kuwa maziwa hayo husaidia katika kumfanya mtu kuwa hodari, mchangamfu na kushinikiza nguvu za kiume, licha ya kwamba haya hayajathibitishwa rasmi kisayansi.

Ni kutokana na faida kama hizi ambazo zimechangia wengi duniani kutafuta na kuanza kutumia maziwa ya ngamia.

Faida 7 za maziwa ya Ngamia:

  • Maziwa ya ngamia yamekithiri zaidi ya maziwa na ng'ombe vitamini C, vitamini B, madini ya iron, calcium, magnesium na potassium.
  • Yametajwa kuwa na uwezo kupunguza uzio dhidi ya baadhi ya vyakula na unojitokeza na misimu.
  • Hupunguza utegemeo kwa insulin na dawa za kutibu kisukari - Imebainika kwamba kunywa maziwa ya ngamia huchangia kupunguzwa kwa dozi ya insulin kwa wagonjwa wa kisukari cha aina ya kwanza.
  • Hushinikiza kinga mwilini - utafiti uliochapishwa katika jarida la utafiti wa bidhaa za maziwa umefichua kwamba kuna viwango vikubwa vya protini katika maziwa ya ngamia baadhi zenye dawa inayoua vidudu mwilini.
  • Hushinikiza ukuwaji - protini nyingi iliomo kwenye maziwa na ngamia tofuati na maziwa na ng'ombe na mbuzi hushinikiza ukuwaji mzuri wa mfupa na ufanyaji kazi wa mifumo ndaniya mwili.
  • Maziwe ya Ngamia yana uwezo wa kusawazisha viwango vya cholesterol mwilini.
  • Madini mengi ya chuma au iron ndani ya maziwa hayo husaidia kuzuia upungufu wa damu mwilini.
Haki miliki ya picha MOHAMED ABDIWAHAB

Je unaweza kunywa maziwa ya Ngamia?

Katika eneo la mashariki ya kati ni kinywaji muhimu cha kitamaduni.

Kiliisaidia waarabu wa kuhama hama wa jamii ya Bedouin kwa karne kadhaa.

Marekani, India, China na Urusi ni mataifa yanaytajwa kuwa masoko makuu ya ukuwaji a maziwa hayo kwa mujibu wa wataalamu.

Licha ya kwamba maziwa haya hutumika sana sana katika mataifa ya Kaskazini na mashariki mwa Afrika na enoe la mashariki ya kati, ripoti ya mwaka 2016 ya serikali ya Australia imetabiri kwamba "miaka mitano kuelekea 2021 kunatarajiwa kushuhudiwa ongezeko la uzalishaji maziwa ya ngamia nchini humo".

Soko la maziwa ya ngamia linazidi kuwa kubwa kutokana na ongezeko la mahitaji ndani na hata nje ya nchi.

Meghan Williams na mumewe Chris walianzisha ufugaji wa ngamia mnamo 2014 waiwa na ngamia watatu ambao iliwabidi wawafunze kukamuliwa maziwa.

Miaka mitano baadaye biashara yao - The Camel Milk Co Australia - imeshamiri mara dufu na sasa wana ngamia 300, 60 katiyao wakitumika kwa kukamiliwa maziwa.

"mara nyingi huwa tunafuatwa na wateja wa kimataifa na masoko yao. Jambo moja tunalojivunia Australia dhidi ya mataifa mengine duniani ni kwamba ngamia wetu hawana magonjwa."

Haki miliki ya picha MEGAN WILLIAMS
Image caption Megan ana mumewe Chris

Ngamia alitumika Australia mara ya kwanza katika miaka ya 1840 kusaidia katika kusafiri katika sehemu kubwa ya nchi hiyo.

Inakisiwa kwamba kuna ngamia milioni 1.2 jangwani.

Baadhi wakiwa ni wa asili ya kiarabu, walio na nundu moja mgongoni na ndio wanaotumika kukamiliwa maziwa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii