Marekani yaiadhibu kwa faini kubwa kwa udukuzi wa taarifa za siri

Tume ya inayolinda maslahi ya watumiaji mtandao huo FTC ilianza kuichunguza Facebook mwezi Machi 2018 juu ya udukuzi wa taarifa za siri Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tume ya inayolinda maslahi ya watumiaji mtandao huo FTC ilianza kuichunguza Facebook mwezi Machi 2018 juu ya udukuzi wa taarifa za siri

Tume ya udhibiti wa masuala ya kibiashara nchini Marekani imeidhinisha faini ya dola bilioni 5 dhidi ya kampuni ya mtandao wa habari wa Facebook kwa ajili ya uchunguzi wa udukuzi wa data binafsi, vinasema vyombo vya habari vya Marekani.

Tume hiyo (FTC) imekuwa ikifanya uchunguzi juu ya madai kwamba taasisi ya ushauri wa kisiasa ya Cambridge Analytica ilipata taarifa kwa njia isiyotakiwa za watumiaji milioni 87wa mtandao wa Facebook.

Malipo hayo yaliiidhinishwa na tume ya FTC kwa kura 3-2, duru zimevihahamisha vyombo vya habari vya Marekani.

Facebook na FTC wameiambia BBC kiuwa hawana la kuzungumzia juu ya repoti hiyo ya uchunguzi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Haijafahamika ikiwa Mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg atachukuliwa hatua zaidi kufuatia faini iliyopigwa kampuni yake

Malipo haya ya faini yalifikiwa vipi?.

Tume ya inayolinda maslahi ya watumiaji mtandao huo FTC ilianza kuichunguza Facebook mwezi Machi 2018 kufuatia ripoti kwamba Cambridge Analytica iliweza kuzifikia taarifa/data za mamilioni ya watumiaji wa mtandao huo wa kijamii.

Uchunguzi huo ulijikita juu ya ikiwa Facebook ilikiuka makubaliano ya mwaka 2011 ambayo kwa mujibu wake ingepaswa kuwafahamisha wazi watumiaji wa mtandao huo na pia ''kuelezea hofu " ya kushirikishadata zao..

Gazeti la New York Times limeripoti kuwa chama cha Democrats kilitaka masharti makali yawekwe dhidi ya Facebook, huku baadhi ya wafuasi wa Democrats wakikosoa kuwa kiwango hicho cha faini hakifai.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Facebook ilikuwa imejipanga kwa malipo ya faini juu ya udukuzi wa taarifa za siri

Facebook imekuwa ikitarajia hatua hii?

Facebook imekuwa ikitarajia hatua hii dhidi yake. Iliwaeleza wachunguzi mwezi Aprili kuwa imetenga kando pesa nyingi kwa ajili ya sakata hiyo , kwa hiyo inamaanisha kuwa kampuni haijtateteleka kifedha kutokana na adhabu iliyopewa.

Kile kisichofahamika ni hatua gani zaidi zitakazochukuliwa au masharti zaidi itakayopewa Facebook, kama vile kuweka mikakati zaidi ya kulinda taarifa za kibinafsi au ikiwa kutakuwa na athari nyingine zai kwa Mkuu wake, Mark Zuckerberg.

Malipo hayo, ambayo ni karibu theluthi moja ya faida nzima ya kampuni, yanaweza kuchochea ukosoiaji kwa wale wanaoweza kusema kuwa kiasi hicho cha fedha ni kidogo

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii