Je ni kweli uhaba wa samaki katika Ziwa Tanganyika unatokana na kupuuza mila na desturi?
Huwezi kusikiliza tena

Uhaba wa samaki Ziwa Tanganyika unatokana na kupuuza mila na desturi?

Nchini Tanzania uvuvi hunufaisha zaidi ya watu milioni nne, huku wakaazi wa mkoa wa Kigoma magharibi mwa Tanzania wakiutegemea kama shughuli kuu inayoendesha Maisha yao kiuchumi.

Hata hivyo shughuli hiyo katika eneo hilo kwa sasa inaenda kombo kutokana na uhaba wa samaki kwenye ziwa Tanganyika huku baadhi ya wavuvi wakiamini kuachwa kwa mila na desturi ni moja ya sababu inayochangia uhaba wa samaki.