Wanawake ''waliobaguliwa'' wamewataka watu kupuuza maneno ya Trump

Rashida Tlaib, Ayanna Pressley, Ilhan Omar na ALexandria Ocasio-Cortez Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Rashida Tlaib, Ayanna Pressley, Ilhan Omar na Alexandria Ocasio-Cortez wakijibu mashambulizi ya 'kibaguzi'

Wabunge wanne walioshambuliwa na rais wa Marekani, Donald Trump, katika mfululizo wa maandishi ya tweeter yanayodaiwa kuwa ya ubaguzi wamepuuza maneno ya rais huyo wakisema ni kujaribu kuwaondoa katika umakini wao.

Wawakilishi hao, Alexandria Ocasio-Cortez, Ilhan Omar, Ayanna Pressley and Rashida Tlaib wamewataka watu wa Marekani kwenye mkutano wa waandishi wa habari ''kutoyatilia maanani'' maneno yake.

Bwana Trump alisema wanawake hao wanne waondoke nchini humo.

Alitetea kauli zake na kukataa shutuma kuwa ni mbaguzi.

Wakizungumza na waandishi wa habari wanawake hao wamesema, hivi sasa watu waweke akili zao kwenye sera za nchini Marekani na si maneno ya raisi Trump.

Kwa pamoja bi Omar na bi Tlaib wamerejea wito wa kutaka bwana Trump apigiwe kura ya kutokuwa na imani yake.

Trump awaambia wabunge wa rangi: 'Ondokeni Marekani'

Trump kuwazuia wanaomkosoa ni 'kinyume cha katiba'

Wanawake hao wamesema nini?

Bi Pressley amezitupilia mbali jitihada za raisi ''kutukandamiza na kutunyamazisha'', akiongeza kuwa walikuwa ''zaidi ya watu wanne.''

''Kikosi chetu ni kikubwa.Kikosi chetu kinahusisha mtu yeyote aliye tayari kujenga ulimwengu wa usawa na haki,'' alisema.

Wanawake wote wanne wamesisitiza kuwa huduma za afya, matumizi mabaya ya silaha, pia kushikiliwa kwa wahamiaji katika mpaka kati ya Marekani na Mexico ni masuala ya kutazamwa.

Bi Omar amesema maneno ya Trump yanadhihirisha kuwa ''mashambulizi ya ubaguzi wa rangi'' dhidi ya wanawake wanne maneno ambayo ''hayana maana yeyote isipokuwa kuigawanya nchi yetu''.

Awali raisi alisema kwa bi Omar alikuwa akiunga mkono kundi la wanamgambo za al-Qaenda. ''Ninajua kuwa kila muislamu aliyeishi nchini humu na duniani kote amesikia kuhusu kauli hiyo hivyo sitaipa nafasi kwa kuijibu,''.aliongeza kuwa hakutegemea jumuia ya watu weupe kujibu baada ya mtu mweupe ''kuua kwenye shule au jumba la sinema, msikiti au sinagogi''.

Bni Ocasio-Cortez alisimulia kuhusu alipotembelea Washington DC akiwa mtoto, akisema watu wawaambie watoto wao kuwa ''chochote kile atakachosema raisi, nchi hii ni yenu''.

Haki miliki ya picha Reuters

Mgogoro umeanzaje?

Siku ya Ijumaa, Bi Ocasio-Cortez, Bi Tlaib na Bi Pressley alitoa ushuhuda mbele ya wabunge kuhusu hali za wahamiaji wanaoshikiliwa kwenye vituo ambavyo walivitembelea.

Wabunge wa Democrat kwa kiasi kikubwa wameushutumu utawala wa Trump hasa namna anavyodhibiti mpaka, wakisema wanawashikilia wahamiaji ambao sasa wana hali mbaya.

Trump amewatetea maafisa wake mpakani .Utawala wake ulitangaza sheria mpya inayoanza kutumika tarehe 16 mwezi Julai, sheria inayokataa kutoa hifadhi kwa mtu yeyote anayevuka mpaka wa kusini ambaye hajaomba kupatiwa hifadhi kwenye ''nchi ya tatu''.

Baada ya ushuhuda huo Trump alitetea kwua hali ya kituo imekuwa ''ikishughulikiwa''. Kisha akatuma mfululizo ujumbe wa twitter kuhusu wanawake na bi Omar.

''Kama huna furaha, ikiwa unalalamika kila kitu unaweza kuondoka,''aliwaambia waandishi wa habari nje ya Ikulu.

Wakati wanawake hao walipokuwa wakiongea na waandishi siku ya Jumatatu, Trump aliandika tena ujumbe wa tweeter kuwa:

''Kama hauna furaha hapa, unaweza kuondoka! ni uamuzi wako, ni uamuzi wako mwenyewe.Hii ni kuhusu mapenzi kwa Marekani,'' aliandika.

Haki miliki ya picha Reuters

Kauli hiyo ilipokewaje?

Bi Pelosi, spika wa bunge, amenukuu ujumbe wa Trump na kutaja maneno yake ya "kibaguzi".

"Wakati @realDonaldTrump anawaambia wabunge wanne wa Marekani warudi nchini mwao, anthibitisha mpango wake wa 'Make America Great Again' unahushu kuifanya Marekani liwe taifa ka watu weupekwa mara nyingine," alisema.

"Utofauti wetu ndio nguvu yetu na umoja wetu ndio nguvu zetu," amesema.

Mada zinazohusiana