Israel: Makaazi ya miaka 9000 yagunduliwa

Maelfu ya vitu, vito vya thamani, mbegu na vifaa vya kilimo vimepatikana katika eneo la jadi la makaazi yaliyodumu kwa miaka 9,000 nchini Israel.

Site of the Neolithic Period settlement near Jerusalem Haki miliki ya picha Israel Antiquities Authority

Wana akiolojia wanaamini eneo hilo ambalo liko karibu na Motza, Magharibi mwa mji wa Jerusalem, wakati mmoja lilikua makaazi ya watu karibu 3,000.

Excavation works Haki miliki ya picha Israel Antiquities Authority

Wachimbaji walipata mabaki ya jengo kubwa lenye vyumba kadhaa ambavyo watu walikua wakiishi wakati mmoja na kupata maeneo mengine ya matambiko yaliokua yakitumiwa na wakaazi hao.

Flint knife Haki miliki ya picha Israel Antiquities Authority

Vitu vingine vilivyopatikana...

Spear head Haki miliki ya picha Israel Antiquities Authority

...ni pamoja ncha ya mkuki uliyotumika kwa shughuli za uwindaji na pengine kujilinda.

Figurine of an ox Haki miliki ya picha Israel Antiquities Authority

Vitu vingine vilipatikana ndani ya kaburi katika kile kinachoonekana kama vifaa vya kufanyia matambiko wakati wa kuzika.

Figurine, depicting a human face Haki miliki ya picha Israel Antiquities Authority
White line 10 pixels

Jiwe hili kinaashiria kichwa cha binadamu.

Bracelet Haki miliki ya picha Israel Antiquities Authority

Bangili tofauti zilizotengenezwa kutokana na mawe pia zilipatikana. Zilikua ndogo kuashiria kuwa zilikuwa zikivaliwa na watoto, watafiti wanasema.

Beads made of obsidian Haki miliki ya picha Israel Antiquities Authority

Vifaa vingine vilivyopatikana glasi vilivyotokana na matope ya moto wa volkeno, kutoka Anatolia.

Excavation site Haki miliki ya picha Israel Antiquities Authority

Mamlaka ya Israel inayosimamia vitu vya kale inasema uvumbuzi huo utabadilisha mawazo ya wanahistoria wa kale katika eneo hilo ambalo liliaminiwa kuwa makaazi ya Yudea enzi hizo.

Picha zote kwa hisani ya Mamlaka ya Israel inayosimamia vitu vya kale.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii