Kuongezeka kwa mimba kwa wanafunzi alaumiwe nani?
Huwezi kusikiliza tena

Kuongezeka kwa tatizo la mimba kwa wanafunzi, 'Nani alaumiwe'?

Nani alaumiwe ni simulizi ya kubuni kusadifu changamoto za ujauzito wanazopata wasichana shuleni.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali nchini Tanzania, zaidi ya wasichana 5,000 walikatisha masomo yao kwa sababu ya mimba mwaka 2016 kutoka wanafunzi 3,000 mwaka 2013. Sasa ongezeko la tatizo la mimba kwa wanafunzi mashuleni, linamfanya Mwalimu Chilu Kiyumbi, kuandika kitabu kinacho akisi tatizo hilo na kutoa mapendekezo ya kulikabili.

Amezungumza na Leonard Mubali.