Ni kwanini Christine Lagarde amejiuzulu kama mkuu wa IMF

Bi Lagarde amesema kuwa ataondoka katika IMF tarehe 12 Septemba Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Bi Lagarde amesema kuwa ataondoka katika IMF tarehe 12 Septemba

Christine Lagarde ameondoka madarakani kama mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Kuondoka kwake mamlakani kunakuja kabla ya uamuzi wa kuteuliwa kuwa mkuu wa benki Kuu ya Muungano wa Ulaya (ECB).

Bi Lagarde amesema kuwa ataondoka katika IMF tarehe 12 Septemba.

" Kwa uwazi uliopo sasa juu ya mchakato wa kuteuliwa kama rais wa Benki kuu ya Muungano wa Ulaya (ECB) na muda utakaochukua, lazima nichukue uamuzi kwa manufaa bora ya Shirika la fedha la kimataifa ," amesema.

" Mkurugenzi mtendaji wa bodi sasa atachukua hatua muhimu zinazohitajika kuendelea na mchakato ewa kumchagua mkurugenzi mpya."

Waziri huyo wa zamani wa Ufaransa amekuwa mkuu wa IMF tangu mwaka 2011.

Ikiwa baraza la Muungano wa Ulaya litaidhinisha uteuzi wake kuongoza ECB , atakuwa ni mwanamke wa kwanza kuwahi kuongoza benki hiyo ya Ulaya yenye jukumu la kuandaa sera ya sarafu ya Euro na masuala ya kifedha kwa ujumla katika nchi zinazotumia sarafu ya Euro.

Akifahamika kama "mwamba nyota" masuala ya fedha ya kimataifa , Bi Lagarde,mwenye umri wa miaka 63, alianza taaluma ya uwakili kabla ya kuingia katika masuala ya kisiasa.

Aihudumu kama waziri wa wizara kadhaa chini ya rais Nicolas Sarközy kabla ya kuchaguliwa kama Mkuu wa kwanza mwanamke wa IMF - akichukua nafasi ya Dominique Strauss Khan.

Je ni nani atayechukua nafasi ya Lagarde katika?

Uteuzi utaanza haraka. Lakini unaibua tena hoja ya mchakato wa zamani wa kumpata uongozi wa IMF na Benki ya dunia.

Kulikuwa na uelewa wa kipindi cha baada ya vita vya pili vya dunia - au dhana kwamba moja kwa moja mkuu wa IMF itachukuliwa na Mtu kutoka Ulaya huku, Marekani wakichukua nafasi ya Mkuu wa Benki ya dunia. Christine Lagarde aliendeleza utamaduni huo.

Alikuwa ni mkurugenzi mkuu wa 5 wa IMF kutoka taifa la Ufaransa. Suala hilo mara ya mwisho lilifichuliwa mapema mwaka huu, wakati nafasi ya kazi ilipojitokeza ghafla ya mkuu wa Benki ya Dunia.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mtu aliyeteuliwa na rais Trump, David Malpass alipata kazi hiyo. Kumekuwa na changamoto juu ya utaratibu huo ulioanzishwa wa kuwapata wakuu wa mashirika hayo muhimu duniani.

Wakati Bi Lagarde alipochaguliwa, Mkuu wa benki kuu ya Mexicoce Agustin Carstens aligombea nagfasi hiyo dhidi yake na alikuwa hajawahi kuteuliwa mtu yeyote kutoka nje ya Ulaya kugombea wadhfa huo awali. Halitakuwa jambo la kushangaza ikiwa wagombea zaidi watajitokeza kugombea nafasi hiyo wakati huu. Hata hivyo kwa sasa vita vya mikataba ya baada ya vita vimesitishwa.

Mara nyingi, Bi Lagarde ambaye amekuwa akiwekwa juu katika orodha ya wanawake 10 wenye mamlaka zaidi duniani amesaidia ku jenga upya uaminifu kwa shirika la IMF baada Ugiriki kupewa dhamana mwaka 2010, ambayo ililegeza masharti ya IMF.

Pia aliongoza utoaji wa dhamana kubwa zaidi ya IMF ya mpango wa dola bilioni 57 kwa ajili ya Argentina mwaka jana.

Mwaka jana , aliripotiwa kusema "hapana, hapana , hapana hapana, hapana hapana " alipoulizwa ikiwa anagombea uongozi wa Benki kuu ya muungano wa Ulaya (ECB).

Hata hivyo, baadae alielezea kupokea uteuzi wake kama "heshima".

Kazi yake mpya huenda ikawa kipimo cha Bi Lagarde ambaye awali alikiri kuwa hana uzoefu wa masuala ya lkiuchumi. Wingu jeusi limetanda juu ya sekta ya benki ya benki ya Utaliano na muungano wa Ulaya unakabiliwa na hatari ya mdololo wa kiuchumi.

Hata hivyo, afisa wa zamani wa IMF amesema kuwa uongozi wake katika masula ya fedha unamaanisha kuwa alikuwa "na uwezo wa kipekee "wa kuongoza Benki kuu ya Muungano wa Ulaya ECB.

Uzoefu wa kazi wa Christine Lagarde

  • 1956: Alizaliwa mjini Paris
  • 1973: Alipata ufadhili wa kusomea katika shule maalum nchini Marekani kwa mwaka mmoja, ambako alipata ujuzi wa kutosha wa lugha ya kiingereza
  • 1981: Paada ya shule ya sheria mjini Paris, alijiunga na kampuni ya sheria ya kimataifa ya Baker & McKenzie kama mshirika, akawa mwenyekiti wake miaka 18 baadae
  • 2005: Alikuwa waziri wa biashara wa ufaransa mwaka 2005
  • 2007: Alikuwa waziri wa fedha wa ufaransa, akiwa mwanamke wa kwanza kuchukua wadfa huo si Ufaransa tu bali miongoni mwa nchi zenye utajiri zaidi wa kiviwanda G8
  • 2011: Alikuwa mkuu wa IMF
  • 2019: Ameteuliwa kuwa rais wa benki kuu ya Muungano wa Ulaya.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii