Unaweza kuiamini kwa kiwango gani FaceApp yenye sura yako?

picha za FaceApp Haki miliki ya picha FaceApp
Image caption Programu imeenea sana- lakini ni mashabiki wake wangapi waliosoma masharti ya matumizi yake?

Kila mmoja anazungumza kuhusu FaceApp - programu inayobadilisha picha za watu za nyuso na kuwaonyesha wakiwa vijana na wazee.

maelfu ya watu wanashirikishana matokeo ya majaribio yao kwa kutumia app kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini tangu mbinu hiyo ya mtandao ya kuhariri picha isambae sana katika siku chache, baadhi wameelezea hofu yao juu ya sheria na mamasharti juu yake

Wanadai kwamba kampuni inatumia njia ya kutojali data za watumiaji - lakini FaceApp ilisema katika kauli yake kuwa picha nyingi zinafutwa kutoka kwenye hifadhi yake saaa 48 baada ya kupakuliwa na mtumiaji.

Kampuni hiyo inasema kuwa iliwahi kupakuwa picha ambazo watumiaji wake walizichagua kuzihariri na sio picha zilizoongezwa.

FaceApp ni nini?

FaceApp si prigramu mpya. kwa mara ya kwanza iligonga vichwa vya habari miaka miwili iliyopita kwa "utambuzi wa asili ".

Hii ilidaiwa kubadilisha uso wa mtu kutoka asili moja na kuifanya kuwa asili nyingine- jambo ambalo lilipingwa vikali na kuondolewa mara moja.

App hiyo inaweza hata hivyo kuondoa au kuongeza kiwango cha mtu anavyotabasamu. Na inaweza kugeuza mitindo ya mapodozi ya mtu.

Haki miliki ya picha Olly Gibbs
Image caption Ap hiyo pia hutumiwa katika uchoraji wa picha

Hii hufanyika kusaidia akili isiyo halis (AI). Mtumiaji huchukua picha ya sura yako na kuirekebisha kwa kutumia picha nyingine.

Hii huwezesha kuingiza tabasamu lenye kuonyesha meno, kwa mfano. wakato anaporekebisha mistari inayozingira mdomo, kidevu na mashavu kwa ajili ya kupata sura mpya

Kwa hiyo tatizo liko wapi?

Wasi wasi ulijitokeza hivi karibuni wakati mtengenezaji wa programu hiyo Joshua Nozzi alipotuma ujumbe wa twitter kwamba FaceApp imekuwa inapakua picha za watu kutoka kwenye simu zao za smartphones bila kuomba idhini.

Hata hivyo mtafiti wa masuala ya usalama wa mtandao wa Ufaransa ambaye Elliot Anderson alichunguza madai ya bwana Nozzi.

Aligundua kuwa hakuna aina ya upakuaji wowote wa picha uliokuwa ukiendelea kutoka kwenye simu za smartphones za watu - FaceApp ailikuwa ikichukua tu picha ambazo watumiaji wake waliamua kuzituma.

FaceApp pia imeithibitishia BBC kwamba ni picha tu ambazo watumiaji wake waliamua kuzituma zinazopakuliwa.

Vipi kuhusu utambuzi wa uso?

Wengine wame shuku kwamba FaceApp inaweza kutumia data zilizokusanywa kutoka kwenye picha za mtumiaji kujifunza utambuzi wa sura.

Hii inaweza kufanyika hata baada ya picha zenyewe kufutwa kwasababu vipimo vya utambuzi wa uso wa mtu vinaweza kuchukuliwa na kutumiwa kwa madhumuni ya aina hayo.

"Hapana, hatutumii picha kwa ajili ya mafunzo ya utambuzi wa sura," Mkurugenzi mkuu wa kampuni , Yaroslav Goncharov aliiamba BBC News. "Ni kwa matumizi tu ya kuhariri picha."

Ni hilo tu?

Hapana. Kuna swali juu ya ni kwanini FaceApp inahitaji kupakua picha wakati programu hiyo inaweza kinadharia kutengeneza picha kwenye smartphones badala ya kuzituma katika cloud.

Kwa FaceApp , hifadhi ya kifaa kama vile simu au kompyuta inayohifadhi picha iko Marekani. FaceApp yenyewe ni kampuni ya Urusi yenye ofisi zake St Petersburg.

Mtafiti wa usalama wa mtandao Jane manchun Wong alituma ujumbe wa twitte kwamba hii inaweza kuifatia FaceApp faida ya ushindani - ni vigumu kwa wengine wanaotengeneza app za aina hiyo kufahamu namna picha hizo zinavyotengenezwa

Je watumiaji wanafahamu yote haya?

Kwa baadhi hiki ndio kiini cha jambo lenyewe. Wakili wa masuala ya kibinafsi Pat Walshe ameainsha jinsi vipengele vya sera ya taarifa za kibinafsi ya FaceApp vilivyoonyesha kuwa huenda data za mtumiaji zinaweza kutambuliwa kwa madhumuni ya kulenga matangazo.

App pia imeambatanishwa na programu ya matangazo - Google Admob, ambayo huwahudumia wa wanaotoa matangazo ya kibiashara kupitia Google.

Bwana Walshe aliiambia BC News kuwa hili lilifanyika "kwa njia ambayo si ya kawaida " na kuongeza kuwa : "Hilo lilishindwa kuwapatia watu njia ya kweli ya kuchagua au udhibiti ." wa matumizi ya app.

Haki miliki ya picha FaceApp
Image caption FaceApp hutoa fursa ya uhariri wa maeneo mbali mbali ya uso

Programu tumishi au app inayotumiwa kufanya hivyo imekumbwa na ukosoaji. Kumekuwa na onyo mbali mbali juu ya namna watumiaji wake wanavyotumia data na wanasiasa nchini Marekani hata wanataka shirika la ujasusi nchini humo FBI kufanyia uchunguzi FaceApp.

Apple yazindua simu mpya ya iPhone X

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii