Kujikimu maisha katika kambi ya wakimbizi
Huwezi kusikiliza tena

Wajasiriamali katika kambi ya Kakuma wenye biashara za mamilioni ya dola

Kwa kawaida kambi za wakimbizi humaanisha uwepo wa maelfu ya watu waliotoroka kuokoa maisha yao na kutegemea msaada wa kigeni. Lakini hali ni tofauti katika kambi ya Kakuma nchini Kenya - kambi ya wakimbizi ya pili kwa ukubwa barani Afrika. Mambo yanabadilika. Watu wanajaribu kutafuta riziki na kujikimu katika maisha yao badala ya kutegemea misaada. Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, uchumi katika kambi hiyo ya wakimbizi una thamani ya dola milioni hamsini na sita huku kukiwepo wateja takriban 180,000.

Video: Anne Okumu/Anthony Irungu

Mada zinazohusiana