FaceApp: Ni vipi ubashiri wake ni sahihi?

Composite image of Arnold Schwarzenegger before the app, after it and what he looks like now Haki miliki ya picha Getty Images/FaceApp
Image caption Arnold Schwarzenegger kabla ya app, baada yake na anavyoonekana kwa sasa

Ni kana kwamba kuna hisia kuwa kila mtu anahisi ameishuhudia FaceApp kwa wakati fulani.

Kurasa zako za mitandao ya kijamii zimefurika picha za watu labda uliosoma nao shule ambazo wanazituma kukuonyesha namna watakavyokuwa wanafanana watakapokuwa wazee.

Programu tumishi au app inayotumiwa kufanya hivyo imekumbwa na ukosoaji. Kumekuwa na onyo mbali mbali juu ya namna watumiaji wake wanavyotumia data na wanasiasa nchini Marekani hata wanataka shirika la ujasusi nchini humo FBI kufanyia uchunguzi app hiyo.

Lakini ni vipi matokeo ya app ni sahihi?

Tuna picha za watu maarufu kuanzia umri wao wa ujana na kupitia picha hizi unaweza kuziangalia na ulinganishe mwenyewe sasa.

Haki miliki ya picha Getty Images/FaceApp/Alamy
Image caption Picha ya Sir Ian McKellen kabla ya app, baada ya app na muonekano wake ulivyo sasa

App kusema kweli imempatia kabisa Sir Ian McKellen aka Gandalf katika filamu ya The Lord of the Rings.

Picha upande wa kushoto ilichukuliwa akiwa na miaka 20 na zaidi mnamo mwaka 1968. Picha ya katikati ni baada ya kupitia mchakato wa FaceApp na iliyopo kulia ni wakati Sir alipocheza filamu ya Magneto katika X-Men: Days of Future Past - akiwa na umri wa 75.

Ilichukuliwa 1965, kushoto Sir David Attenborough akiwa na umri wa miaka 39. Picha ya katikati ni matokeo ya picha yake baada ya kupitia mchakato wa app na kulia ni mapema mwaka huu akiwa na umri wa miaka 93.

Dolly Parton

Haki miliki ya picha Getty Images/FaceApp
Image caption Dolly Parton kabla ya app, baada na namna anavyoonekana sasa

Haya si matokeo mazuri sana ya App

Kushoto mwimbaji huyo wa muziki wa country Dolly Parton alipokuwa na miaka 30 -1977. Katikati ni baada ya kupitia mchakato wa app na kulia ni mapema 2019, akiwa na umri wa miaka 73.

Unaweza kusema muonekano wake wa sasa wa uzee ni bora zaidi kuliko ulivyotengenezwa na app.

Dame Judi Dench

Haki miliki ya picha Getty Images/FaceApp
Image caption Dame Judi Dench kabla ya app, baada na namna anavyoonekana kwa sasa

Kushoto , mchezaji filamu wa muda mrefu Dame Judi Dench akiwa na umri wa miaka 33 mwaka 1967. Katikakati muonekano wa app. Kulia ni mwaka 2019, akiwa na umri wa miaka 84.

Kusema ukweli, hatudhani James Bond asingefurahia sana matokeo ya app.

Arnold Schwarzenegger

Haki miliki ya picha Getty Images/FaceApp
Image caption Arnold Schwarzenegger kabla ya app, baada yake na anavyoonekana kwa sasa

Pocha ya kushoto ni ya ujana ya mchezaji filamu wa Austria anayeitwa Arnold Schwarzenegger iliyochukuliwa mwaka 1976. Picha ya katikati ni ya baada ya kufanyiwa mchakato wa app. Kulia, ni ya mwanasiasa makini Arnold Schwarzenegger iliyochukuliwa mwaka 2019 akiwa na umri wa miaka 74.

FaceApp ni nini?

FaceApp si programu mpya. Kwa mara ya kwanza iligonga vichwa vya habari miaka miwili iliyopita kwa "utambulizi wa asili ".

Hii ilidaiwa kubadilisha uso wa mtu kutoka asili moja na kuifanya kuwa asili nyingine- jambo ambalo lilipingwa vikali na kuondolewa mara moja.

App hiyo inaweza hata hivyo kuondoa au kuongeza kiwango cha mtu anavyotabasamu. Na inaweza kugeuza mitindo ya mapodozi ya mtu.

Hii hufanyika kusaidia akili isiyo halisi (AI). Mtumiaji huchukua picha ya sura yako na kuirekebisha kwa kutumia picha nyingine.

Hii huwezesha kuingiza tabasamu lenye kuonyesha meno, kwa mfano. Wakati anaporekebisha mistari inayozingira mdomo, kidevu na mashavu kwa ajili ya kupata sura mpya.

Picha za FaceApp zimewavutia sana watu mbali mbali katika eneo la Afrika mashariki. Hawa ni baadhi yao walioweka picha zao mtandaoni wakionyesha sura zao watakapokuwa wazee:

1.Salim kikeke mwandishi wa BBC idhaa ya kiswahili:

2.Msanii wa muziki wa Kenya al maarufu Akothee:

Unaweza pia kusikiliza:

Huwezi kusikiliza tena
Habari za Global Newsbeat 1000 21/12/2017

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii