Patrick Odhiambo: Hakimu 'aliyechangisha pesa' kumuokoa mwanamke aliyeiba nywele bandia Kenya

Mahakamani Haki miliki ya picha Getty Images

Hakimu mkuu mkaazi wa mahakama ya Shanzu mjini Mombasa Pwani ya Kenya Patrick Odhiambo, amekonga nyoyo za Wakenya kwa kutumia ''busara'' kuamua kesi ambapo mshukiwa alikiri kosa la kuiba nywele bandia katika duka moja la jumla hivi karibuni.

Kwa mmujibu wa Mtandao wa Runinga ya K24 nchini Kenya Hakimu Odhiambo ilichukua hatua hiyo baada mshukiwa kwa jina Karyn Chelagat, 19, kukiri kosa la wizi na kusema alitamani kuwa na muonekano wa marafiki zake lakini hakuwa na uwezo.

"Nilatamani kuwa na muonekano mzuri kama wanawake wengine. kwa hio, nilienda duka la jumla kutafuta nywele za bandia ambazo mara nyingi marafiki zangu hutumia. Nilizipata lakini nilivunjika moyo kwani sikuweza kumudu bei yake. Sikua na budi ila kuiba, bidhaa hiyo," Chelagat aliiambia mahakama huku akidondokwa na machozi.

Mshukiwa huyo aidha alimwambia hakimu kuwa umasikini "umemfanya ashindwe kujitunza vizuri".

"Nimelelewa katika umasikini. Nilipokuja mjini, Niliona wanawake warembo mimi piaa nilijaribu kadiri ya uwezo wangu kuwa na muonekano kama wao lakini ukosefu wa fedha ulininyima fursa hiyo ," alisema Chelagat.

Ni wakati huo ambapo hakimu aliwaomba mawakili katika mahakama hiyo na wakenya wengine kumchangia Chelagat angalau shilingi 100 ili aweze kulipa deni la shilingi 1,140 alizokuwa anadaiwa na mlalamishi.

Moja wa mawakili, William Bosire, alitoa shilingi 2,000 ali kumuokoa mwanamke huyo kutokana na kifungo cha miaka miwili gerezani kutokana na kosa hilo.

La sivyo mshukiwa angelilazimika kulipa faini ya shilingi elfu 50,000 ili aachiliwe kwa dhamana.

Hakimu mkuu Odhiambo alimuachilia huru Bi Chelagat na kuwaagiza maafisa wa uchunguzi wa kesi hiyo kurejesha nywele hizo kdukani na halikadhalika 2000 zilizotolewa na wakili zikapewa mshtakiwa ''akanunue nywele alizotaka na chakula".

Kisa hicho kulizua gumza miongoni mwa Wakenya katika mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter huku wengi wao wakipongeza hatua ya hakimu Odhiambo wakisema ''huo ndio utu''

Kongowea Mswahili aliandika katika ukurasa wake wa Facebook: "Kwa hiyo, watu wenye utu na moyo wa huruma wapo Kenya? Maajabu."

Patrick Maina Kamanga aliandika : "Kumbe, tuna watu walio na utu kiasi hii hata [Mahakamani]. Mungu ambariki hakimu, natoa wito mfumo wetu wa sheria ufuate mfano huu mwema."

Wengine kama Elizabeth Akinyi aliandika katika Twitter yake akisema, wazo lake lilikuwa kuomba mchango wa kumsaidia binti huyu.

Pastor Dan Kim aliandika : Hii ndio Kenya tunayotaka''

Jim Nick Muigai alisema : "Huu ni ubinadamu. Hakimu alitumia busara kubwa kuamua kesi hii. Binti huyu sasa anatakiwa atathmini maisha yake upya manake ameponea kwenye tundu la sindano."

Martin Francis alimuunga mkono hakimu akisema: "Sio lazima tuangangatie yaliyoandikwa kwenye vitabu kuamua kesi. Fanya uamuzi mwafaka ndio sababu umepewa cheo hicho."

Reuben Karanja alisena: "Huu ndio ungwana unaongozwa na busara, unamfanya mtu ajirudi mwenyee badala ya kumuadhibu (aliye na makosa)

Mishieni Misheni ambaye hakuchelea kuelezea furaha yake aliandika : "Kusema kweli sikutarajia hilo kabisa… Nimeamini watu wema wapo. Hakimu amemtendea jambo la kitu mwanadada huyo!"

Lakini sio kila mmoja aliyesifia uamuzi huo wa Hakimu Odhiambo.

Khamati Khamati alilaani kitendo hicho akisema: "Hatua hii haifai kabisa. Hawa ni wezi wa kawaida wanaofanya uhalifu halafu wanasingizia hali zao za kimaisha. Kuna msemo usemao mtu hujikuna ajipatapo, usipoweza kuzingatia sheria utalipia madhambi yako. Hii ni makosa."

Orrorin Samuels alisema: "Hii ni kinyume na sheria. Hakimu amefanya kosa akiwa katika kazi yake rasmi ."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii