Kamati ya kupambana na Ebola yaidhinishwa Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo baada ya waziri wa Afya Oly Ilunga kujiuzulu

Oly Ilunga. Photo: 15 July 2019 Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Oly Ilunga ametaja ukiukaji wa maadili na kuingiliwa kati kazi yake katika barua ya kujiuzulu

Serikali Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeidhinisha kamati ya kuratibu muitikio wa serikali katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola mashariki ma nchi hiyo.

Hatua hiyo imeidhinishwa saa chache baada ya mhusika aliyeongoza jitihada hizo kwa muda wa mwaka uliopita kujiuzulu.

Waziri wa afya Oly Ilunga amejiuzulu katika kulalamikia namna ambavyo mlipuko huo wa Ebola unavyoshughulikia nchini.

Baadhi kutoka ikulu wanaona Dkt Ilunga amejiuzulu kutokana na tuhuma kwamba alikataa kuwashirikisha wengine katika mapambano dhidi ya ugonjw ahuo.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Oly Ilunga ameshutumu uamuzi wa rais Félix Tshisekedi kumteua muu mwingine wa kikosi kinachokabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini.

Ameshutumu pia alichokitaja kuwa shinikizo la nje la kuidhinihsa chanjo za majaribio kwa ugonjwa huo.

Mlipuko huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,700 katika mwaka uliopita.

Suali kubwa ni kamati hiyo inatarajiwa kuleta tofuati gani katika mapambano dhidi ya Ebola nchini?

Wiki iliyopita shirika la afya duniani (WHO) lilitangaza kwamba mlipuko wa ugonjwa huo kuwa dharura ya afya ya kimataifa.

Janga la ugonjwa wa Ebola liliathiri sehemu kadhaa za Afrika magharibi kuanzia 2014 hadi 2016, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 11,000.

Kwanini Ilunga anajiuzulu?

Katika barua yake kwa rais Félix Tshisekedi, ameshutumu uamuzi wa kumuondoa yeye kama kiongozi wa kikosi kinachokabiliana na Ebola nchini na badala yake kuchaguliwa kamati ilio "chini ya usimamizi wako binafsi".

Amesema wanakamati hao waliingia kazi yake katika miezi ya hivi karibuni.

Ameshutumu pia "shinikizo kubwa lililopo katika miezi ya hivi karibuni" kutumia chanjo ya majaribio ya Ebola inayopigiwa upatu na mashirika ya misaada na wafadhili.

Amesema chanjo iliopo sasa ndiyo iliothibitishwa kufanyakazi pekee.

Hali ni mbaya kiasi gani Congo?

Mlipuko wa hivi sasa - wa pili kwa ukubwa - ulianza mnamo Agosti mwaka jana na umeathiri majimbo mawili nchin iCongo , Kivu ya kaskazini na jimbo la Ituri.

Zaidi ya watu 2,500 wameathirika na ugonjwa huo huku thuluthi mbili ya idadi hiyo wakiwa wamefariki.

Huwezi kusikiliza tena
Je inawezekana kuangamiza virusi vya Ebola?

Imechukua siku 224 kwa idadi ya visa kufika 1,000, lakini siku 71 za zaidi kwa idadi hiyo kufika 2,000.

Visa 12 vipya vinaripotiwa kila siku.

Je chanjo inafanya kazi ?

Ndio. Kwa 97% na zaidi ya watu 161,000 wamepewa chanjo hiyo kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.

Hatahivyo sio kila mtu aliopewa chanjo hilo, ni wanaokaribiana moja kw amoja na wagonjwa wa Ebola na watu wengine waliogusana nao.

Muitikio kwa mlipuko hu wa sasa umetatizwa kwa mashambulio ya mara kwa mara dhidi ywa wahudumu wa afya , na imani potofu kuhusu chanjo inayotolewa sasa.

Iliidhinishwa wakati wa janga lililoshuhudiwa Afrika magharibi na imetumika wakati wote wa mlipuko huu wa sasa.

Ebola ni nini?

Haki miliki ya picha BSIP/Getty Images
  • Ebola ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi ambapo aliyepata maambukizi hupata dalili za homa, uchovu, maumivu ya viungo na koo.
  • Kisha mgonjwa hutapika, kuharisha na kutoka damu.
  • Watu huambukizwa kwa njia ya kugusana, njia ya mdomo na pua, pia kwa njia ya damu, matapishi, kinyesi,majimaji ya kwenye mwili wa mtu mwenye Ebola
  • Wagonjwa hupoteza maisha kutokana na kupungukia maji mwilini na viungo kushindwa kufanya kazi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii