Wafahamu wanawake watano waliobobea kisayansi

Haki miliki ya picha Schmidt Futures/BBC/NovoNordisk/Getty

Mwanamke mhandisi aliyeshiriki katika kazi ya kutua mwezini ameongea wiki hii kuhusu namna alivyoambiwa wakati mmoja kuwa chumba cha udhibiti wa vyombo vya safari za anga za mbali sio mahala pa wanawake . Mambo yamebedilika sana miaka 50 iliyopita, lakini sio kwa kiwango ambacho baadhi walikitumaini. BBC imezungumza na wanasayansi kutoka vizazi tofauti ambao wamevunja vizuizi katika kazi zao za kisayansi.

Muanziilishi : Profesa Jocelyn Bell Burnell

Maarufu kwa uvumbuzi wa kwanza wa kidogo cha anga kinachofahamika kama-pulsar kinachotuma mawimbi ya sauti ya redio zaidi ya miaka 50 iliyopita, Prof Dame Jocelyn Bell Burnell pia amekuwa mtetezi wa muda mrefu wa wanawake katika sayansi.

Akiwa mtoto wa shule katika Ireland kaskazini miaka ya 1950, kama wasichana wengine hakuruhusiwa kusoma masomo ya sayansi hadi wazazi wake na watu wengine walipopinga.

"Wavulana walipelekwa katika maabara ya sayansi na wasichana walikuwa wanapelekwa katika chumba cha sayansi kimu kwasababu kila mtu alifahamu kuwa wasichana walikuwa wanajiandaa kuolewa kwahiyo walihitaji kujifunza jinsi ya kutandika kvitanda," anakumbuka.

Haki miliki ya picha Colin McPherson
Image caption Dame Jocelyn Bell Burnell

Wanawake watano wanaoutikisa ulimwengu wa sayansi

Akiwa Profesa wa masomo ya fizikia ya anga katika Chuo Kikuu cha Oxford, alikuwa ni mmoja wa wanawake wanasayansi ambao juhudi zao ziliwezesha kutolewa kwa tuzo za kutambua mchango wa wanawake wenye taaluma ya juu katika sayansi. Mpango wa Athena Swan unavitaka vyuo vikuu na vyuo kutatua tatizo la usawa wa jinsia katika sayansi.

Mgawanyo wa kijinsia katika sayansi ni wa kitamaduni zaidi kuliko uwezo wa kiakili wa mwanamke na baadhi ya nchi zinafanya vema kuliko nyingine, anasema.

katika fizikia ya ya vyombo vya anga nchi za kusini mwa bara la Ulaya kama Ufaransa, na Italia zimefanya vema zaidi kuliko mataifa ya kaskazini mwa bara la Ulaya kama vile Ujerumani na Uholanzi, kwa mfano.

"Katika nchi zote idadi ya wanawake wanaojiunga na fani hiyo ya sayansi inaongezeka lakini hali imesalia kuwa kama ilivyo , jambo ambalo linafurahisha," anasema.

"Mafanikio ni ya taratibu, mambo yanabadilika polepole."

Ushauri wake kwa wanawake katika sayansi anasema? "Usitishwe, endelea kuwemo ndani, fanya kazi kwa bidii na bila shaka uwe jasiri."

Kiongozi wa utafiti : Dkt Nicola Beer

Mapenzi ya Dkt Nicola Beer ya sayansi yalianza wakati alipokuw ana umri mdogo ; moja ya kumbukumbu zake za zamani zaidi ni kumtizama mwalimu wake akijaribu kuelezea dhana ya mawimbi ya sauti kwa kutumia kipande cha karatasi kilichojazwa mchelena kipaza sauti katika shule yao ya msingi.

Akiwa ndiye mtu wa kwanza wa familia kusoma masoma ya Chuo kikuu, shahada yake ya kemia ya baiolojia katika Chuo Kikuu cha Bristol ilimuwezesha kupata Shahada ya uzamivu(PhD) katika chuo Kikuu cha Oxford a na kupata udhamini wa kimasomo nchini Marekani katika MIT na Harvard kabla ya kuongoza timu ya watafiti.

Haki miliki ya picha NovoNordisk
Image caption Dr Nicola Beer

Akiwa mkuu wa idara ya Uvumbuzi wa Kibaiolojia & Kifamasia katika kituo cha Novo Nordisk katika chuo kikuu cha Oxford, ni mkuu wa idara na sayansi.

"Ni suala la kupanga mkakati wa muongozo, kuwasaidia watu kuboresha mawazo yao, kuyatekeleza na pia kuwaunga mkono katika kazi zao ," anasema.

Anaamini kuwa kwa wanawake wachache sana walio katika nafasi za uongozi , wanawake wanawajibu wa kuungana mkono , kama wa washauri, kwa kueneza ujuzi , au kwa kuwa tu '' wakarimu na kufungua milango ".

"hicho ndio kitu ninachofikiri tunapaswa kuwa tunakifanya wanawake wote iwe ni wanawake , au vijana , au iwe ni watu katika safari zao zao za kikazi . Tuna wajibu wa kutengeneza njia ya jinsi mambo yatakavyokuwa kuliko kulinda tu vyeo vyetu , na ni muhimu tufanye hilo kwa ukarimu ," anasema.

Kama mwanamke kiongozi , alibaini kwamba mara nyingi watu hujaribu kupendekeza njia zinazofanana kwa ajili ya wanawake za wanawake kuwa viongozi , kama vile kuwa wenye kupaza sauti au kuwa wasemaji zaidi katika hali au kujibu mambo kwa njia ambayo iliyopoangwa.

"Ninadhani tunapaswa kuweka juhudi pamoja za kuwatia moyo wanawake kuwa viongozi bora wawezavyo , kuliko kuwanyanyapaa kuhusu jinsi wanavyopaswa kuelekar ," anasema.

Kwake , hii inamaanisha kuepuka dhana za awali ambazo tunaweza kuwa nazo kati yetu ,kama vile kuweka vikomo kwa yale tunayoweza kufanikiwa, au kwa yale tunayoweza kuyafanya.

Mvumbuzi : Gladys Ngetich

Wakati Gladys Ngetich alipoambiwa kwenye mkutano kuwa , 'huonekani kama mhandisi ,' alikwenda nyumbani akijiuliza mhandisi anapaswa kuwa na sura gani.

Kama mwanafunzi wa utafiti akisomea uhandisi mitambo alikuwa amezowea kupambana na unyanyapaa na kuwa kitu ambacho ni cha uvumbuzi . Akisoma shahada ya uhandisi mitambo nchini Kenya alikuwa ni mwanafunzi pekee wa kike kati ya wanafunzi 80.

Haki miliki ya picha Schmidt Futures
Image caption Gladys Ngetich

Anasema mwaka wake wa kwanza , "wengi miongoni mwa wanafunzi wa kiume walidhani sitaweza ",lakini alifaulu kwa alama za juu katika shahada yake.

Hili karibuni alimaliza masomo yake ya shahada ya uzamivu- PhD katika uhandisi wa utengenezaji wa ndege na vyombo vya anga za mbali katika Chuo kikuu cha Oxford, alishinda tuzo ya mwaka 2019 ya sayansi -Schmidth Science Fellowship kwa kuchunguza teknolojia za sayansi ya anga zinazosaidia maendeleo ya kudumu.

Akiiga mfano wa wanawake kama Profesa Bell Burnell, anataka kuwa mfano kwa vizazi vipya vya wahandisi.

Huwezi kusikiliza tena
Wanawake watano wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani

"Ninatumai kutakuwa na orodha ya wanawake watakaokuja baada yangu - na ni matiumaini yangu kuwa hawatahitajika kujithibitisha kupita kiasi

Dkt Megan Wheeler

Ni vipi unatatua changamoto kubwa zinazoikabili dunia ? Sayansi ina majibu , lakini kama tu utaliangalia tatizo kwa taswira tofauti . Hayo ndio maoni ya Dkt Megan Wheeler,ambaye kama Mkurugenzi mkuu mtendaji wa mpango wa HS Schidt Sience Fellowship ana mpango wa kuwapatia mafunzo wanasayansi wa kizazi kipya.

Haki miliki ya picha Schmidt Futures
Image caption Dr Megan Wheeler

Dkt Wheeler ana shahada mbili za uzamivu ya sayansi ya ubongo katika chuo kikuu cha Oxford na saikolojia ya kliniki aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Marekani . kwa sasa anaongoza mpango unaolenga kuwanoa wanasayansi wenye akili zaidi na wanaokuwa wa kwanza katika kukabilianana changamoto za dunia.

Kazi kama vile mradi wa kubaini jeni za biandamu imeonyesha thamani ya kufanya kazi kwa kuvuka mipaka ya tamaduni katika sayansi, anasema

"Ninadhani kuwa ni muhimu kwamba tuwe na wanasayansi ambao si wenye uzoefu wa kina tu bali wawe pia na uwezo wa kuvuka mipaka yote hiyo ," alifafanua.

Kuwa mwanasayansi leo inamaanisha kuwa na uwezo wa kutoka nje ya maabara na kuwasiliana na watu juu ya ni kwanini kazi unayoifanya ni muhimu ,anasema.

Nyota inayopanda:Elina Aino Johanna Pörsti

Akiwa ni binti wa mwalimu wa fizikia na daktari , Elina Aino Johanna Pörsti alikulia nchini Finland katika familia iliyokuwa na mazungumzo ya kisayansi. Radi ilipopiga , baba yake alikuwa akiwaelezea fizikia nyuma ya radi , huku mama yao akiwaelezea kuhusu umbo la binadamu.

kama mtoto alionyesha moyo wa ujasiliamali , wakati alipofungua duka lake la dawa kwneye eneo la mwambao.

Haki miliki ya picha BBC/Helen Briggs
Image caption Elina Aino Johanna Pörsti

Shuleni alisomea masomo ya baiolojia katika uhariri wa jeni , ambayo yalimtayarisha kwa ajili ya kazi yake ya baadae.

" Ni jambo la kufurahisha kwamba ungeweza kuondoa vinasaba-DNA na kufanya kazi katika maabara na nilifikiri ilikuwa ni jambo linalisikika kuwa zuri sana na kitu ambacho ningekifanya," anasema.

" Kwangu mimi binafsi ninavutiwa na sayansi kwasababu ninapenda kuelewa , na huwa kuna mengi wakati wote ya kuelewa na kuna mengi wakati wote ya kusoma na kujifunza."

Alisomea sayansi ya masi katika Chuo kikuu cha Helsinkina akapata shahada ya uzamili ya biashara kutoka Copenhagen. Kwa sasa ni mwanasayansi katika taasisi ya utafiti wa kisayansi ya Novo Nordisk ya Oxford akishughulia uvumbuzi wa vifaa vya utambuzi wa magonjwa.

Anasema katika shule nchini Finland,kila mtu alikuwa sana , jambo ambalo ni muhimu katika kuimarika kwa wanawake katika sayansi.

"IKatika kufikiria jinsi ya kuimarisha nafasi ya wanawakekatika sayansi kwa ujumla ninadhani kazi inapaswa kuanza mapema ," anasema Elina.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Mwanamke ana nafasi gani katika kubadilisha maisha Tanzania?

Follow Helen on Twitter.

Mada zinazohusiana