Vichanga vyaokolewa kwa Benki za maziwa ya mama
Huwezi kusikiliza tena

Umuhimu wa maziwa ya mama: Wanawake wachangia akiba ya maziwa kuokoa vichanga Kenya

Maziwa ya mama yanatajwa kuwa muhimu sana katika maisha ya mtoto hususan punde baada ya kuzaliwa.

Japo ni jambo la kawaida kwa wanawake kuwanyonyesha watoto wao baada ya kujifungua kwa baadhi hilo huja na changamoto zake. Wanawake wanaojifungua watoto njiti ambao muda wao wa kuzaliwa haujafika mara nyingi hawana maziwa.

Nchini Kenya wanawake ambao wanajifungua watoto na kuwa na maziwa mingi kupita kiasi, wameanza kuwagawia wenzao wasiyo kuwa nao.

Mpango huu unafanyika katika hospitali kuu ya kujifungulia akina mama ya Pumwani mjini Nairobi.

Video: BBC Maisha