Uingereza: Waziri Mkuu mpya kuunda serekali baada ya kupewa idhini na Malkia

Boris Johnson Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Boris Johnson ataingia Downing Street kwa mara ya kwanza kama Waziri Mkuu

Boris Johnson ataanza mchakato wa kuunda serikali yake baada ya kuapishwa rasmi kupokea wadhifa wa Waziri Mkuu kutoka kwa Theresa May.

Kiongozi huyo mpya wa Conservative atachukuwa rasmi hatamu ya uongozi baadae leo Jumatano baada ya kukutana na Malkia katika Ikulu ya Buckingham Palace.

Baada ya kuingia Downing Street, anatarajiwa kutangaza sehemu ya Baraza lake la mawaziri, ikiwa ni pamoja na waziri wa fedha na wa yule wa usalama wa ndani.

Vyanzo vya habari karibu na Bw. Johnson vinaripoti kuwa viongozi wa ngazi ya juu watakuwa wale wanaoegemea uongozi wa "Uingereza ya sasa".

Pia anatarakiwa kuchukua nafasi hiyo kuongeza idadi ya wanawake katika baraza la Mawaziri na kuimarisha uwakilishi wa makundi ya jamii zilizotengwa.

Bw. Johnson alimshinda mpinzani wake Jeremy Hunt kwa kura 92,153 dhidi ya 46,656.

Katika hotuba yake baada ya ushindi huo, Meya huyo wa zamani wa mji wa London aliahidi kuwa "ataiwasilisha Brexit, kuiunganisha nchi na kumshinda Jeremy Corbyn".

Akizungumza mjini London, alisema: "Tutaipa nchi nguvu.

"Tutaiwasilisha Brexit kufikia Oktoba 31 na kuchukua fursa zote zitakazotokana na muamko mpya wa inawezekana.

"Tutajiamini upya na tutainuka upya na kuondosha shaka na fikra za kutojiamini."

Takriban wanachama 160,000 wa Conservative walikuwa na fursa ya kupiga kura na katika waliojitokeza ni 87.4%.

Asilimia ya kura kwa Johnson - 66.4% - ilikuwa chini ya aliyojishindia waziri mkuu wa zamani David Cameron mnamo mwaka 2005 aliyejinyakulia 67.6%.

Mashauriano ''yanaendelea'' kati ya Bw. Hunt na Johnson kuhusu wadhifa wa waziri mpya wa Mambo ya nje.

Waziri Mkuu mpya anatarajiwa kulihutubia taifa kwa mara ya kwanza nje ya Downing Street baada ya kupata idhini ya kubuni serikali kutoka kwa Malkia.

Hatua mbayo itafuatia ni Theresa May kuwasilisha rasmi barua yake ya kujiuzulu kama Waziri MKuu katika Ikulu ya Buckingham Palace.

Uchambuzi wa Laura Kuenssberg, Mhariri wa BBC wa kisiasa

Boris anaipokea serikali ambayo haina uwingi, ilio na siasa ziliyoachanganyika na sera ambayo katika miaka mitatu ijayo Uingereza na Brussels imeshindwa kuitatua.

Na yeye ni mwanasiasa, ambaye hata washirika wake wanaoshangazwa na kipaji chake wanakiri hung'ang'ana kutoa maamuzi kwa wepesi.

Kauli ambayo inaweza kufurahisha au kuogopesha. Kauli ambayo anaeleza kwamba miezi 12 iliyopita hata wafuasi wake sugu hawange weza kuliamini hilo.

Lakini sio kauli kavu tu, pengine sio jambo la kawaida kisiasa, ambalo huenda lisikere kwa namna yoyote.

Kwa vyovyote vile unvayomtazama Boris Johnson, yeye ni mwanasiasa ambaye sio rahisi kumpuuza.

Huyu ni mtu ambaye hata utotoni mwake alitaka kuwa 'mfalme wa dunia'.

Sasa ni mfalme wa chama ha Conservative, na wanaoipigia upatu Brexit, ndio mahakimu.

Ratiba ya mambo yatakavyokuwa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Malikia Elizabeth II

Jumatanokuanzia 12:00 BST kuendelea: Theresa May atajibu maswali ya wabunge kwa mara ya mwisho kama Waziri Mkuu.

Baada ya chakula cha mchana atatoa hotuba fupi Afnnje yaNo 10 kabla ya kwenda kukutana na Malkia ili amkabidhi barua yake ya kujiuzulu.

Baada ya hapo Boris Johnson atawasili Ikulu ya Buckingham Palace ambako atapewa idhini ya kuunda serikali.

Kisha atahutubia taifa nje ya jengo la Downing Street kabla ya kuingia ndani ya jumba hilo kwa mara ya kwanza kama Waziri Mkuu.

Baadae, ataanza kutangaza uteuzi wa mawaziri, kama vile wa Fedha, Mambo ya ndani na waziri wa Mambo ya nje, na kisha kupiga na kupokea simu ya kwanza kutoka kwa viongozi wengine duniani.

Alhamisi: Bw Johnson anatarajiwa kulihutubia bunge kuhusu mpango wake wa Brexit na kujibu maswali kutoka kwa wabunge.

Baadae Bunge litaenda mapumziko lakini Waziri Mkuu mpya ataendelea kutangaza baraza lake la mawaziri.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii