Je mgogoro wa Iran utaathiri mfuko wako kiuchumi?

Kituo cha mafuta Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption AA inasema kwamba bei ya petroli nchini Uingereza mwezi Julai ziko juu tangu 2014

Huku joto la wasiwasi likipanda baada ya Iran kuikamata meli iliokuwa ikipeperusha bendera ya Uingereza katika Ghuba, kumekuwa na msukusuko wa bei ya mafuta, hatua inayozua hofu ya kupanda kwa bei ya petroli katika siku chache zijazo.

AA imeonya kwamba mgogoro huo wa muda mrefu kuhusu usalama wa meli za kimataifa zinazobeba mafuta kupitia mkondo wa bahari wa Hormuz unaweza kupandisha bei ya mafuta ya Uingereza msimu huu.

Na Uingereza tayari imeionya Iran kwamba huenda kukawa na athari mbaya za kidiplomasia iwapo haitaiachilia meli ya Stena Impero ikiashiria kwamba huenda kukawa na athari mbaya katika siku zijazo.

Petroli hutengezwa kutoka kwa mafuta na tishio la kusambaza mafuta hayo huenda likachochea bei ya mafuta kupanda kwa watumiaji.

Je mgogoro wa Iran unaathiri vipi bei ya mafuta?

Iran iliikamata meli ya mafuta ya Sterno Impero kulipiza kisasi kukamatwa kwa meli ya mafuta ya Iran iliokuwa ikipeleka mafuta Syria , lakini hatua hiyo inajiri kufuatia hali ya switofahamu kati ya Marekani na Iran ambao wameshutumiana kwa uchokozi katika eneo hilo.

Katika muda huo wote , Tehran imedaiwa kushambulia meli sita nyengine za mafuta katika mkondo wa Hormuz , hatua iliofanya meli za wanamaji wa Marekani na Uingereza kupiga kambi katika eneo hilo.

Kuna hofu kwamba Iran huenda ikajaribu kuufunga mkondo huo wa bahari , ambao ni njia muhimu ya meli za mafuta, hatua ambayo inaweza kuzuia mafuta kutoka katika eneo la Ghuba.

Hatua hiyo intarajiwa kupunguza moja kwa tano ya mafuta yote duniani mbali na robo ya gesi yake aslia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Iran iliikamata meli iliokuwa ikipeperusha bdenra ya Uingereza

Wengi wanaamini kwamba suluhu ya kidiplomasia ndio itakayoafikiwa.

Hatahivyo iwapo Iran itaufunga mkondo wa bahari wa Hormuz itasababisha bei ya mnafuta kupanda kwa kiwango cha juu , kulingana na David Balston, mkuu wa biashara ya uchukuzi wa meli nchini Uingereza.

Kuna vituo vingine vya mafuta nje ya eneo la Ghuba lakini ni vidogo kwa hivyo utalazimika kutafuta masoko kwengine.

''Hatua hiyo itaongeza bei ya mafuta na gesi nchini Uingereza'', anaongezea, kwa kuwa asilimia 5 ya mafuta ya taifa hilo na asilimia 13 ya gesi yake aslia hupitia katika mkondo wa Hormuz.

''Na bila suluhu ya kidiplomasia , hatua hiyo huenda ikasasabisha jibu la kijeshi kutoka kwa washirika wake wa magharib''i, anasema.

Ni nini kinachofanyika na bei ya mafuta?

Bei za mafuta kote ulimwenguni zimekuwa na msukosuko katika wiki za hivi karibuni kutokana na mgogoro unaoendelea, lakini haujakuwa mbaya zaidi, anasema John Hall, mwenyekiti wa kampuni ya nishati ya Alpha Energy Group consultancy.

Pipa moja la mafuta ghafi lilikuwa likiuzwa $63.5 siku ya Jumatatu ikiwa ni zaidi ya $10 chini ya bei yake ya mafuta ya juu 2019.

Bwana Hall anadhania kwamba hili litaathiri kwa ukubwa soko ambalo huamua bei ya mafuta ambalo kwa sasa limechoka kutokana na vitisho kutoka kwa rais wa Marekani Donald Trump dhidi ya Marekani.

Hadi kufikia hivi majuzi , kila wakati ambapo rais Trump alikua akichapisha ujumbe wa Twitter, kulikuwa na mabadiliko katika soko lakini wawekezaji walikuwa na kinga, alisema bwana Hall.

Badala yake wawekezaji wanatazama vyanzo katika soko hilo la mafuta ambavyo sio vizuri.

Uchumi wa China unashuka hivyobasi mahitaji kutoka kwa taifa la pili duniani linalotumia mafuta kwa wingi huenda yakapungua.

Na jaribio la shirika la muungano wa mataifa yanayouza mafuta duniani Opec kama vile Saudia pamoja na Urusi kuongeza bei ya mafuta kupitia kupunguza kiwango cha usambazaji wa mafuta duniani liliambulia patupu kutokana na ongezeko la uzalishaji wa bidhaa hiyo kutoka Marekani.

Kuna uwezekano kwamba kiwango cha mafuta kote duniani kitaongezeka katika kipindi chote cha mwaka kilichosalia hatua inayotarajiwa kudhibiti bei ya mafuta, kulingana na bwana Hall.

Haki miliki ya picha Getty Images

Je hii inamaanisha nini kwa bei ya mafuta?

AA inasema kwamba bei za mafuta za Uingereza mwanzoni mwa msimu huu zilikuwa za juu tangu 2014 zikiwa asilimia 128.5 kwa lita ya petroli na asilimia 131.7 kwa lita ya dizeli.

Mkuu wa Kampuni ya nishati ya Alpha Energy Group bwana Hall anasema kuwa Iran haiwezi kufunga mkondo wa Hormuz , lakini iwapo itafanya hivyo huenda ikasababisha tatizo kubwa la ukosefu wa mafuta na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo hadi $ 100 kwa pipa.

Iwapo mambo yangekuwa mabaya zaidi bei ya petroli ingepanda hadi asilimia 20 kwa lita , anasema.

Hatahivyo hatua muhimu ni jinsi Uingereza itajibu kukamatwa kwa meli ya Stena, anasema .

Kwa sasa kuna makabiliano ya kidiplomasia kati ya Iran, Marekani na Uingereza huku Iran ikidaiwa kuwa ndio inayofanya uchokozi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii