Bobi Wine kukabiliana na Museveni uchaguzi wa 2021 Uganda

Bango la mbunge wa Kyadondo mashariki Bobi Wine

Mbunge wa Kyadondo mashariki nchini Uganda Bobi Wine ametangaza azma yake ya kuwania urais nchini humo 2021.

Amezindua kikosi kitakacho endesha kampeni yake ya kuwania urais 2021.

Umaarufu wake miongni mwa vijna nchini Uganda unaonekana kama changamto kwa kiongozi mkongwe Yoweri Museveni.

Museveni, mwenye umri wa miaka 74, anatarajiwa kuwania muhula wa sita madarakani.

Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, anakabiliwa na mashtaka ya uhaini baad aya kukamatwa mwaka jana kufuatia kupurw amawe msafara wa rais baada ya mkutano wa kisiasa.

Anadai kwamba aliteswa na kupigwa akiwa kizuiziki mnamo Agosti, jamboa ambalo maafisa wa serikali wanalikana.

Mwanamuziki huyo ambaye hivi majuzi alijiunga na siasa amethibitisha kwamba atampinga rais Museveni katika kinyang'anyiro cha urais kama mgombea huru na hivyobasi kumaliza uvumi uliokuwa ukienea kuhusu uamuzi wake.

''Tuliamua kwamba tutaupinga utawala huu'' , Bobi wine aliambia gazeti la Financial Times siku ya Jumatatu baada ya kuzungumza na shirika la habari la AP kwamba atawania urais.

Aliliambia gazeti la Financial Times kwamba zaidi ya wabunge 50 , ikiwemo 13 kutoka kwa chama tawala cha rais Museveni cha National Resistant Movement NRM waliunga mkono ugombeaji wake na hivyobasi kumpatia ujasiri wa kuogombea kiti hicho.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii