Manny Pacquiao amchokoza Floyd Mayweather akitaka pigano la marudiano

Floyd Mayweather na Manny Pacquiao Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Floyd Mayweather (kushoto) alimshinda Manny Pacquiao katika pigano la mwisho lake la mwisho dhidi ya pacquiao 2015

Floyd Mayweather amemwambia Manny Pacquiao kukumbuka kwamba yeye ndio 'bwana mkubwa' baada ya raia huyo wa Ufilipino kumpatia changamoto ya pigano la marudio.

Mayweather mwenye umri wa miaka 42 alihudhuria pigano la ushindi la Pacquiao dhidi ya Keith Thurman lakini akasema kwamba alihudhuria pigano hilo kwa sababu za kibiashara kwa kuwa Pacquiao amesainiwa chini ya mshauri wake Al haymon.

''Nilikuwa katika pigano lako nikikushauri ,mfanyikazi wangu'', aliandika katika instragram. Akimkumbusha pigano lao la 2015, aliongezea, ''Nilikupiga kiakili, kimaungo na kifedha''!

Mayweather alifananisha pato alilojipatia la $9m baada ya kushinda pigano la maonyesho baada ya sekunde 139 dhidi ya Tenshin Nasukawa na fedha alizojipatia Pacquiao dhidi ya ushindi wake na Thruman.

''Ulijipatia $10m kwa raundi 12, wakati mimi nilijipatia $9m chini ya dakika 3 nilipocheza na muwasilishaji Piza'', aliongezea. Jina la mtu huyu limejengwa kwa kutumia jina langu na ni wakati muwache kutumia jina langu kujipatia ufuasi''.

''Najua hamupendelei jinsi kijana mweusi aliyewacha shule ya upili aliwashinda nyote kiakili na kustaafu akiwa hajashindwa huku nikiweza kudhibiti jina langu kwa kufanya chaguo bora mbali na kuwekeza vyema''.

Pacquiao, 40, ambaye anahudumu kama seneta nchini Ufilipino alimtaka Mayweather kufufua pigano lao la 2015 ambalo liliweka historia kubwa baada ya ushindi wake dhidi ya Thurman.

Haki miliki ya picha Manny Pacquiao
Image caption Floyd Mayweather amemwambia Manny Pacquiao kukumbuka kwamba yeye ndio 'bwana mkubwa' baada ya raia huyo wa Ufilipino kumapatia changamoto ya pigano la marudio.

Mayweather alishinda pigano hilo kwa wingi wa pointi na wengi waliamini kwamba hawezi tena kukabiliana na Pacquiao katika pigano ambalo litahatarisha rekodi yake ya mapigano 50 bila kushindwa.

Afisa mkuu mtendaji wa Mayweather Promotions na mshirika wake mkubwa , wiki iliopita amesema kuwa Mayweather hana hamu na pigano la pili, huku mkufunzi wa Pacquiao Freddie Roachi akisema kuwa haoni pigano hilo likifanyika.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii