Safari ya kutisha ya uvumbuzi wa bidhaa ya mpira duniani

wafanyakazi wa shamba la mpira jamii ya Bongwonga Haki miliki ya picha Anti-Slavery International
Image caption wafanyakazi wa shamba la mpira jamii ya Bongwonga

Picha isiyo na rangi inawaonyesha wanaume wakiwa wanaonekana wakimtazama pengine mpiga picha au mtu mwingine, ni vigumu kueleza.

Picha hii ilipigwa mwaka 1904 na watu waliokuwa kwenye safari ya kimisionari eneo la Baringa nchini Congo. Mwanaume mmoja kwa jina Nsala na mkewe na watoto waliuawa.

Haki miliki ya picha Anti-Slavery International
Image caption Mmisionari na mpiga picha Alice Seeley Harris wakivuka daraja nchini Congo

Charles Goodyear, aliingia kwenye madeni wakati biashara ya familia yake ilipoingia kwenye madeni, lakini alipanga kujinasua kwenye hali hiyo. Wazo lake likawa kuboresha aina ya mpira ambao utaweza kufanya kazi baada ya kujaza upepo.

Haki miliki ya picha Getty Images

Kwa bahati mbaya, Meneja alipenda wazo lake la mpira wa upepo- lakini alikiri kuwa kampuni yake ilikuwa katika hali mbaya.

Hakuwa peke yake. Wawekezaji wote nchini Marekani waliweka pesa yao kwenye uvumbuzi mpya- wa mpira uliokuwa ukivutika, usiopitisha upepo, wenye kukunjika na usiopitisha maji- lakini mambo hayakuwa mazuri kwa upande wake.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kadi ya picha inayoonyesha watu wakirina mpira

Mwaka 1820, kiasi kikubwa cha mpira kilikuwa kikipelekwa duniani kote kutoka nchini Brazil, kutokana na bidhaa hiyo yalitengenezwa makoti, kofi na viatu.Kisha kilifika kipindi cha joto na wajasiriamali walishuhudia kwa mshangao ugunduzi wao ukigeuka kuwa kero kutokana na harufu mbaya ya bidhaa ya ngozi.

Kulikuwa na fursa ya mafanikio makubwa kwa yeyote ambaye angeweza kutengeneza bidhaa ya mpira yenye kuhimili joto na baridi. Kweli, Goodyear hakuwa mtaalamu wa kemia hakuwa na fedha pia, lakini kwa nini hivi viwe vikwazo?

Kwa miaka kadhaa aliongozana na mkewe Clarissa na watoto kutoka mji mmoja kwenda mwingine, wakipanga nyumba zilizo duni, wakiweka rehani mali walizokuwa nazo, kutokana na madeni.

Charles alianza utafiti wake kwa kutumia vyombo vinavyopikiwa chakula, akichanganya mpira na kila kitu kilichokuja akilini mwake kama magnesium, limao, Carbon.

Mhandisi wa Tanzania atuzwa na WHO kwa uvumbuzi wake

Makaazi ya miaka 9000 yagunduliwa

Hatimaye alipata jibu: kuunguza mpira na Sulphur. Hii hivi sasa kisayansi inaitwa (vulcanisation).

Katika kulinda hakimiliki, Charles alilazimika kukopa fedha zaidi, na kwa bahati mbaya alifariki akiwa na deni kiasi cha pauni 161,000.

Lakini alikuwa ameiweka bidhaa ya mpira katika ramani nzuri kama moyo wa uchumi wa viwanda. Mpira ulitengeneza vitu mbalimbali kuanzia kwenye mavazi, mipira ya kumwagilia maji mpaka bidhaa za magari na kwa ajili ya vifaa vya umeme.

Mwishoni mwa miaka ya 1880, mgunduzi wa Uskoti, John Dunlop alibuni sehemu ambayo aliona kuna mapungufu ambacho ni tairi la kujaza upepo, ambalo awali lilishawahi kutengenezwa lakini bila mafanikio.

Alikuwa akitumia baiskeli ya kijana wake akijaribu kuitazama upya namna ya kuiboresha kwa kuiwekea kitu laini mithili ya mto. Watengenezaji wa baiskeli wakaona kuna faida kwenye uvumbuzi huo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mtoto wa John Dunlop akiwa kwenye picha na baiskeli ya kwanza yenye magurudumu yenye upepo

Baadhi ya vitu vimebadilika tangu Nsala alipokutana na Seeley Harris kijiji cha Baringa. Zaidi ya nusu ya zao la mpira duniani sasa halitoki kwenye mti bali mafuta.

Jaribio la kutengeneza mpira lilianza baada ya mpira halisi kuwa maarufu. Wakati wa vita ya pili ya dunia bidhaa hiyo iliondoshwa baada ya Asia kuvunja usambazaji wa bidhaa, Serikali ya Amerika ililazimisha viwanda vyake kutengeneza bihaa mbadala. Mpira uliotengenezwa kwa kemikali gharama yake ni ya chini na wakati mwingine ni bora zaidi kwa mfano, kwa ajili ya magurudumu ya baiskeli.

Na wakati tunatengeneza magari, malori na ndege zaidi, tunahitaji bidhaa ya mpira zaidi kuvisha matairi yake, na hilo ni jambo gumu.

Miti inayotupatia bidhaa ya mpira inaathiriwa kimazingira, hivyo wataalamu wa mazingira wanahofu kuhusu upungufu wa maji.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wafanyakazi wakivuna mpira nchini Cambodia

Ukisafiri umbali wa kilometa 1000 kwenye msitu mnene kutoka Baringa, ambako Seeley Harris alikutana na Nsala, utafika katika eneo la Meyomessala nchini Cameroon, sehemu ya Hifadhi ya Dja Faunal, ambayo Unesco ilitangaza kuwa eneo la urithi

Kampuni kubwa duniani ya usindikaji bidhaa ya mpira Halcyon Agri inasafisha maelfu ya ekari kwa ajili ya miti ya mpira katika mashamba ya Sudcam.

Makundi ya wanaharakati wa mazingira wakiwemo Greenpeaze, WWF na kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya misitu walipaza sauti kuhusu hatari ya ukataji miti katika eneo hilo. Pia kuhusu baadhi ya wanakijiji kupatiwa fedha za fidia baada ya kupoteza ardhi zao.

Mwaka 2018 , Halcyon Agri ilitangaza kushughulikia changamoto hizo nchini Cameroon.

Mada zinazohusiana