Boris Johnson ndiye waziri mkuu mpya wa Uingereza aliyemrithi May

Boris Johnson
Image caption Boris Johnson, waziri mkuu mpya wa Uingereza

Boris Johnson amesema anataka ''kubadili Uingereza'' akishakuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.

Akiongea nje ya Dawningstreet, amesema Uingereza itaondoka kwenye Umoja wa Ulaya tarehe 31 mwezi Oktoba ''hakuna shaka'' kuhusu hilo.

Wale wote wenye ''mashaka'', na wanaosema kuwa jambo hili halitafanikiwa ''wamekosea'', alisema waziri mkuu mpya.

Pia ameahidi kushughulikia suala la maslahi ya wazee ''mara moja''.

Boris Johnson kuwa Waziri Mkuu mpya Uingereza

Nani kushinda Uwaziri Mkuu wa Uingereza leo?

Marekani na Uingereza zarushiana cheche za maneno - kunani?

Bwana Johnson amemrithi Theresa May ambaye amewasilisha nyaraka za kujiuzulu kwake mbele ya Malkia muda mfupi uliopita.

Waziri Mkuu muda mfupi baadae ataunda baraza lake-idadi kadhaa ya mawaziri wa bi May wamejiuzulu, wakisema kuwa hawawezi kufanya kazi chini ya utawala wa bwana Boris.

Boris amesema Uingereza itaondoka Umoja wa Ulaya ndani ya siku 99.

Lakini pia ameahidi kuongeza uwekezaji kwenye kuboresha miundombinu ya usafiri na elimu na pia kuboresha huduma za afya.

Image caption Mwenza wa Boris Johnson Carrie Symonds na washirika wake wengine

Bwana Johnson ameapa kuyaleta mataifa yote manne ya Uingereza pamoja ili kuupa nguvu mpango wa Brexit wa nchi hiyo.

''Ingawa sasa ninajenga timu ya wanaume na wanawake, nitawajibika katika kuleta mabadiliko ninayotaka kuyaona,'' alieleza.

Awali, akiachia madaraka baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu, Bi May amesema imekuwa ''heshima kubwa kwake'' na kumtakia kila la heri mrithi wake.

Katika hotuba yake, amesema mafanikio ya serikali yake ni mafanikio ya nchi nzima.