Utafiti: Kwa nini watu ni waaminifu kuliko tunavyofikiria

Wallet Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jumla ya pochi 17,000 'ziliangushwa' katika miji 355 ya nchi 40

Miaka kadhaa iliyopita mtafiti mmoja "alipata" vipochi 400 katika maeneo tofauti ya umma kama vile Benki, ukumbi wa Sinema, Hotelini, Mahakamani na hata katika vituo vya polisi katika miji minane ya India.

Watu waliotumwa na mtafiti huyo waliviwasilisha kwa walinzi wa maeneo hayo au wahudumu wanaokaribisha wageni na wakidai wameviokota njiani.

Baadhi ya vipochi hivyo havikuwa na hela na vingine vilikua na dola zaidi ya dola tatu pesa taslimu.

Kila kipochi kilikuwa na kadi tatu zinazofanana za biashara zilizo na jina la mwenyewe na anwani yake ya barua pepe, orodha ya vitu alivyotaka kununua na ufunguo.

Siku chache baadae kundi la watafiti waliojidai kuwa wenye vipochi hivyo walisubiri kupigiwa simu na hao walinzi kama sehemu ya utafiti wa kubaini kiwango cha uaminifu wao.

Vipochi hivyo vilikabidhiwa wanaume 314 na wanawake 86 katika miji ya Ahmadabad, Bangalore, Coimbatore, Hyderabad, Jaipur, Kolkata, Mumbai na Delhi.

43% ya vipochi vilizokuwa na pesa viliwasilishwa kwa wenyewe. lakini zile hazikuwa na hela ni kidogo sana zilizoripotiwa kupatikana- 22% pekee ndio zilizowasilishwa kwa wenyewe.

Matokeo ya utafiti huu wa kushangaza uliochapishwa hivi karibuni katika Jarida la kisayansi, unathibitisha kuwa watu ni waaminifu kuliko vile ''tunavyofikiria''

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waleti 400 wallets "ziliangushwa" katika miji minane ya India ili kubaini kiwango cha uaminifu wa watu katika miji hiyo

Alain Cohn, mtaalamu wa saikolojia ya tabia katika Chuo Kikuu cha Michigan na ambaye pia ni mmoja wa watafiti hao anasema "Hatukutarajia tulichokiona".

"Watu wanapojua kuwa huenda wakafaidika kotokana na tabia ya kutokuwa na uaminifu, hamu ya kuficha ukweli inaongezeka lakini usumbufu wa kiakili unaoandamana na hisia ya kujiona mwizi huwafanya kubadili mawazo - hasa ikiwa hawajazoea kuiba kitu cha mtu," watafiti wanasema.

Mji wa Kusini mwa India,ulikua na kiwango cha chini cha watu walioripoti kuokota vipochi vilivyokuwa na pesa - Bangalore (66%) na Hyderabad (28%).

Mji wa Coimbatore, uliandikisha idadi kubwa ya watu walioripoti kuokota vipochi ambavyo havikuwa na hela (58%), huku mji mkuu wa Delhi, ukiwa na kiwango cha chini cha wale waliorudisha vipochi ambayo havikuwa na hela(12%).

Watafiti waligundua kuwa wanawake walifurahia sana kuwasilisha vipochi walivyookota viwe na pesa au la - wakilinganishwa na wanaume.

Utafiti wa ''kuangusha'' kipochi ama vipochi nchini India ilikuwa sehemu ya utafiti mkubwa wa Kimataifa uliofanywa na watafiti ili kubaini tofauti kati ya uaminifu na maslahi ya kibinafsi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waleti nyingi zilizzo okotwa hazikuwa na pesa

Kati ya mwaka 2013 na 2016, watafiti "waliangusha" jumla ya vipochi 17,000 katika miji 355 ya nchi 40.

Baadhi ya vipochi hivyo vilikuwa na pesa- $13.45 ambazo zimebadilishwa katika sarafu za nchi husika na kuongezwa kiwango chake kulingana na kiwango cha maisha cha watu wa nchi hiyo.

Miji mitano kati ya nane kubwa zilishirikishwa katika utafiti huo.

Watafiti walikadiria kuwa watu katika mataifa 38 kati ya 40 watarudisha vipochi vilivyo na hela. (mataifa mawili ambao waleti hazikurudishwa ni Peru na Mexico.)

Lakini kiwango cha pesa kilipoongezwa mara saba zaidi katika waleti hizo na kuangushwa tena katika mataifa matatu, kiwango cha waleti zilizorudishwa kilipanda kwa 18%.

Waleti zilizokuwa na pesa nyingi zilirudishwa kwa kiwango kikubwa Denmark (82%) na kiwango cha chini kutorudisha ilikuwa (13%).

Switzerland (73%) na China (7%) zilikuwa na kiwango cha juu na cha chini cha kurejeshwa kwa waleti ambazo ziliokotwa bila kuwa pesa ndani.

Kupima kiwango cha uaminifu wa mtu ni hali ngumu sana

Utafiti huo ulibaini mambo mengi kuhusu tabia za watu tofauti. Kwa mfano mlinzi ambaye anasimamia usalama wa jengo fulani India alitaka tumhonge ili ashiriki utafiti huo.

Tulifahamu baadae kuwa hakuwasiliana na mwenye kipochi. Katika sehemu nyingine mwanamume tuliyempatia kipochi hicho hiyo alisema tumwachie hiyo wale na kwamba pesa zilikuwa ndani anatizipeana kama sadaka ikiwa hatafanikiwa kumpata mwenyewe.

"Nitaandika barua pepe ikiwa sitapokea mawasiliano yoyote kutoka kwa mwenyewe baada ya kumtaarifu, [Nitawapatia waliona uhitaji]. bila shaka hii ni sawa na rushwa," alisema.

"Ni jambo la kufurahisha sana kubaini kuwa watu wanakuwa waaminifu zaidi kimataifa ikiwa kitu walichookota kinahusisha pesa taslimu ," Dr Zünd alisema. "Hilo lilijitokeza sana India na mataifa mengine ya bara Asia."

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Denmark ilikuwa na kiwango cha juu cha watu walioripoti vipochi vilivyokuwa na pesa

Kwa ufupi utafiti huu unatufunza nini?

Matokeo ya utafiti huu yanaashiria wazi kuwa binadamu huwajali binadamu wenzao wawe wanajuana au la.

Ndio maana wengi wao waliripoti kuwa wameokota vipochi - cha kufurahisha ni kwamba vipochi vingi vilivyokuwa na ufunguo vilirejeshwa kuliko vile ambavyo havikuwa na ufunguo.

Zaidi ya yote, kuna "athari ya kisaikolojia" inayomfanya mtu kujiona kama mwizi.

"Ni rahisi kwa mtu kutojiona kuwa muaminifu akiamua kuchukua kipochi ambacho hakina pesa kwa sababu hajafaidika na lolote.

Lakini inakuwa vigumu pesa ikihusishwa katika mjadala huo," anasema Dr Zünd.

Vipi na wale ambao hawakutoa ripoti kuwa wameokota kipochi?

Wanauchumi wanasema huenda wakawa si watu waaminifu , lakini huenda pengine wamepatwa na shughuli nyingi au wamesahau kipochi chenyewe

Uaminifu bila shaka ni sera nzuri ya maisha ya kila mwanadamu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii