Kwa nini chanjo ya Ebola inapingwa DRC?

Wakati mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ukiendelea kurindima katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mbunge mmoja mashariki mwa nchi hiyo amepinga matumizi ya chanjo mpya itakayotumika kama jaribio la kutibu ugonjwa wa Ebola.

Muhindo Nzangi Butondo anasema haifai kwa wakazi wa eneo lake wanatumika kwa majaribio ya chanjo hizo mpya.

Awali aliyekuwa Waziri wa Afya Dokta Oly Ilunga pia alitofautiana na Rais Felix Tshisekedi kuhusu chanjo hiyo.

Lakini kwa nini baadhi ya viongozi na raia wanapinga awamu hii ya pili ya chanjo ya Ebola?

Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda, amezungumza na Dufina Tabu,mwanaharakati wa Shirika la kijamii lijukikanalo kama ASVOCO.