Jordan imezindua makavazi ya kwanza ya kijeshi chini ya bahari

Gari al kivita aina ya kifaru iliyozamishwa futi 92 chini ya bahari Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gari al kivita aina ya kifaru iliyozamishwa futi 92 chini ya bahari

Jordan imezindua makavazi yake ya kwanza ya kijeshi chini ya bahari katika pwani ya Aqaba.

Katika hafla ya uzinduzi huo siku ya Jumatano, ufalme huo ulizamisha magari kadhaa ya kivita pamoja na helikopta kijeshi chi ya bahari.

Magari hayo yameegeshwa kana kwamba yako vitani yamewekwa katika miamba ya matumbawe yaliopo chini ya bahari nyekundu.

Mamlaka zinasema onyesho hilo ni mbinu mpya ya utalii kwa wageni wanaozuru taifa hilo.

Miamba ya matumbawe katika sehemu ya Kaskazini mwa Bahari nyekundu ni kivutio kikubwa kwa wapiga mbizi na watalii wengine.

Halmashauri ya eneo maalum la kiuchumi la Aqaba (ASEZA) imeongeza kuwa itajumuisha aina tofauti ya michezo katika "mazingira hayo ya maonesho".

Helikopta ya kijeshi, iliyotolewa na kikosi cha jeshi la hewa la Jordan, ilikuwa moja ya vyon=mbo vya kijeshi vilivyozamishwa chini ya bahari Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Helikopta ya kijeshi, iliyotolewa na kikosi cha jeshi la hewa la Jordan, ilikuwa moja ya vyon=mbo vya kijeshi vilivyozamishwa chini ya bahari
Halmashauri ya eneo maalum la kiuchumi ya Aqaba imeiambia Jordan Times kuwa ma vifaa hatari vilitolewa ndani ya magari hayo kabla yazamishwe Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Halmashauri ya eneo maalum la kiuchumi ya Aqaba imeiambia Jordan Times kuwa ma vifaa hatari vilitolewa ndani ya magari hayo kabla yazamishwe
Jordanian Armed Forces' armoured vehicle lies on the seabed of the Red Sea off the coast of the southern port city of Aqaba Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watakaoweza kuzuriu makavazi hayo ni wapiga mbizi wanaotumia vifaa maalum na wataliii wanaotumia maboti maalum yalio na sakafu ya kio
Wapiga mbizi wakitoka ndani ya maji baada ya kuzamisha magari ya kijeshi chini ya bahari nyekundu katika pwani ya Aqaba Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiga mbizi wakitoka ndani ya maji baada ya kuzamisha magari ya kijeshi chini ya bahari nyekundu katika pwani ya Aqaba

Picha zotye zina haki miliki.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii