Trump akaidi uamuzi wa bunge na kuamua kuiuzuia silaha Saudi Arabia zenye thamani ya $8bn

Rais Trump, akiwa pamoja na mwanamfalme wa Saudia wanashika chati inayoonyesha mauzo ya silaha kwa Saudia katika ikulu ya White House tarehe 20 Machi 2018 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Trump, akiwa pamoja na mwanamfalme wa Saudia wanashika chati inayoonyesha mauzo ya silaha kwa Saudia

Rais huyo wa Marekani ametumia kura ya turufu kufutilia mbali uamuzi wa bunge la Congress la kuzuia mauzo ya silaha yenye thamani ya $8bn kwa Saudia na UAE.

Donald Trump alisema kuwa maamuzi hayo matatu yatadhoofisha uwezo wa Marekani ulimwenguni na kuharibu uhusiano wake na washirika wake .

Hatua hiyo inajiri baada ya mabunge yote mawili kupiga kura ya kuzuia mauzo hayo.

Baadhi ya wabunge wanasema kwamba walihofia kwamba silaha hizo huenda zikatumiwa dhidi ya raia katika mgogoro wa Yemen.

Wameshutumu vitendo vya Saudia nchini Yemen pamoja na mauaji ya mwaka jana ya mwandishi Jamal Khashoggi.

Hatahivyo bunge le seneti litapiga kura baada ya siku moja ili kuona iwapo litakaidi uamuzi wa bwana Trump , kulingana na kiongozi wa wengi katika chama cha Republican Mitch Connel.

Lakini wachanganuzi wanasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba bunge la seneti halitakuwa na thuluthi tatu ya kupinga uamuzi huo wa Trump

Ni mara ya tatu kwa bwana Trump kutumia uwezo wake tangu alipochukua mamlaka

Mnamo mwezi Mei , Ikulu ya Whitehouse ilitangaza hali ya dharura ya kitaifa kukaidi uamuzi wa wabunge hao na kupitisha mauzo hayo ya silaha.

Wakati huo Bwana Trump alisema kuwa alifanya uamuzi huo kutokana na vitisho vinavyotolewa na Iran.

Lakini hatua hiyo ilizua upinzani mkali kutoka kwa wale waliohofia kwamba silaha hizo zitatumiwa dhidi ya raia nchini Yemen na vikosi vya Saudia.

Wabunge wakiwemo wale wa Republican katika bunge la Seneti pia walisema kwamba kulikuwa hakuna sababu muhimu ya kukaidi maamuzi ya Congress.

Hatahivyo akitumia kura yake ya turufu , bwana Trump alipendekeza kwamba kuzuia uuzaji wa silaha hizo kutaendeleza mgogoro wa Yemen kwa muda mrefu na kwamba raia wengi wataathirika nchini Yemen.

Pia alisisitiza kuwa Saudia na UAE zinapinga vitendo vya Iran na washirika wake katika eneo hilo.

Hali ya wasiwasi kati ya Marekani na Iran imeongezeka tangu rais Trump ajiondoe katika makubaliani ya kinyuklia ya Iran ili kuzuia mpango wa kinyuklia wa Iran.

Marekani inasema kwamba iliangusha ndege isio na rubani ya Iran wiki iliopita na imelaumu Iran kwa msururu wa mashambulizi dhidi ya meli za mafuta katika Ghuba.

Iran iliangusha ndege isio na rubani ya Marekani mwezi Juni.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii