Matapeli wa mitandaoni
Huwezi kusikiliza tena

Jinsi matapeli 'wanavyowaliza' watu kwenye simu

Kutokana ukuaji wa teknolojia ya simu za mikononi kwa kuunganika na huduma za kifedha, uhalifu wa kimtandao nao umechupa.

Mataifa kama Tanzania na Kenya katika ukanda wa Afrika Mashariki yalilazimika mpaka kutunga sheria ili kudhibiti uhalifu huo, lakini bado haujakoma.

Watu hufanya udanganyifu na utapeli wa mitandao na wapo ambao hupata nambari za simu za watu na kuweza kupiga kwa nia ya kuwalaghai.

Wengine hutuma ujumbe wa kutaka kutumiwa fedha ambapo ikiwa mtu alikua na miadi na mtu basi mara moja hufanya muamala akiamini ni mtu mwenye makubaliano nae

Mwandishi wa BBC Leonard Mubali aliweza kuwanasa watu ambao moja kwa moja huwezi kukwepa kusema ni matapeli baada ya kumpigia simu huku wakitaka kufanya nae biashara fulani.

Aliwafuatilia na kunasa sauti zao wakati wa mazungumzo yao tangu awali, isikilize taarifa yake kwa kina.

Mada zinazohusiana