Kwa nini Kenya inataka wajumuisha watu wenye jinsia mbili kwenye sensa?

Nembo ya - male, i marker and female
Image caption Makundi ya kutetea haki yanakadiria kuna watu zaidi ya 700,000 wenye jinsia mbili Kenya

Kenya itakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kukusanya data ya watu wenye jinsia mbili katika sensa ya kitaifa.

Sensa hiyo ya iliyopangiwa kufanyika mwezi wa Agosti inalenga kubaini idadi ya watu ambao hawajitambulishi kama wanaume au wanawake.

Mahuntha nchini Kenya hushambuliwa mara kwa mara na kubaguliwa katika jamii.

Watu hao wanakadiriwa kuwa zaidi ya 700,000 miongoni mwa wakilinganishwa na idadi jumla ya watu milioni 49 nchini Kenya.

"Kupata taarifa kuhusu watu wenye jinsia mbili katika sensa ni itatusaidia kuelewa changamoto tunazopitia," alisema Ryan Muiruri, mwanzilishi wa chama cha watu walio na jinsia mbili nchini Kenya (IPSK), akipongeza hatua hiyo ya serikali.

"Kujumuishwa katika sensa ni hatua kubwa sana kwetu," aliiambia BBC.

Afrika Kusini ilikuwa taifa la kwanza la Afrika kuwajumuisha watu walio na jinsia mbili katika sheria inayopinga ubaguzi.

Mwanzoni mambo yalikuaje?

Mwaka 2009, mwanamke mmoja raia wa Kenya aliwasilisha kesi mahakamani kutaka ufafanuzi baada ya daktari kuandika kutoa ishara ya kutofahamu jinsia ya mtoto wake katka stakabadhi zake.

Alitaka ufafanuzi wa vitu vitatu: iStakabadhi inayotambulisha jinsia ya mtoto wake ili aweze kwenda shule, sheria ya kuziua mtoto aliye na jinsia mbili kufanyiwa upasuaji wa kimatibabu hadi pale hatua hiyo itachukuliwa kwa kuzingatia umuhimu wa kiafya, na maelezo sahihi na kuwasaidia kumawazo wazazi walio na watoto mahuntha.

Katika uamuzi wa kihistoria kuhusu kesi hio mwaka 2014, mahakama Kuu iliiagiza serikali kumpatia mtoto huyo wa miaka mitano cheti chake cha kuzaliwa.

Huwezi kusikiliza tena
Darlan Rukih: Nilibaguliwa kwa kuwa na jinsia mbili

Mahakama hiyo pia ilimuagiza mwanasheria mkuu kubuni jopokazi maalum ambalo litatathmini njia bora zaidi ya kuwasaidia watoto waliozaliwa na jinsia mbili.

Jopo hilo liliwasilisha mapendekezo yake kwa mwanasheria mkuu mwezi Aprili mwaka huu.

Baadhi ya mapendekezo hayo ni kuchelewesha upasuaji wa kimatibabu hadi pale mtoto atakapokuwa na kujiamulia jinsia anayotaka na kufanyika kwa utafiti wa kubaini idadi yao halisi nchini Kenya.

Pia lilipendekeza kujumuishwa kwa alama ya inatambulisha jinsia yao katika stakabadhi zote za umma.


Jinsia mbili

Ni neno linalotumiwa kuwaelezea watu wanaozaliwa na matatizo ya kibaolojia katika jinsia zao ambazo haziwezi kutajwa kuwa upande wa kike au kiume.

Kuna aina tofauti inayohusu viungo nyeti, ovari, korodani na homoni.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa karibu asilimia 1.7 ya watu wako hali hiyo duniani.

Nalo Shirika la Afya Duniani, linasema kuwa kuna aina 42 tofauti ya watu wenye jinsia mbili ulimwenguni.

Ijapokuwa hakuna takwimu zilizokusanywa kuhusu hili, wataalamu wanasema kuwa, kwa kila watoto elfu 20 wanaozaliwa, mmoja ana jinsia mbili.


Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii