Korea Kaskazini yatoa onyo kwa Korea Kusini kwamba ni vigumu kujilinda dhidi ya kombora lake jipya

Kombora la korea kaskazini Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Korea kaskzini ilirusha makombora yake mawili katika bahari ya Japan

Korea Kaskazini imetaja majaribio ya makombora yake mapya siku ya Alhamisi kuwa onyo rasmi dhidi ya kile ilichokitaja kuwa uchokozi wa Korea Kusini.

Kombora hilo la masafa mafupi lilirushwa katika bahari ya Japan , pia ikijulikana kama bahari ya magharibi kutoka Wonsan katika pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini.

Kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un alisema kuwa taifa lake lililazimika kuunda silaha ili kukabiliana na tishio la moja ka moja.

Amesema kuwa jaribio hilo lilishirikisha mfumo wa kiufundi wa kuelekeza makombora.

Matamshi ya bwana Kim yalioripotiwa katika vyombo vya habari yanajiri baada ya Korea Kaskazini kukosoa uamuzi wa Korea Kusini na Marekani kushiriki katika zoezi la pamoja la kijeshi mwezi ujao.

Korea Kaskazini imetaja zoezi hilo la kijeshi kama maandalizi ya kulivamia taifa hilo.

Ijapokuwa Marekani na Korea Kusini zimekataa kufutilia mbali zoezi hilo la kila mwaka, wamepata pigo.

Mkuu wa majeshi wa Korea kaskazini amesema kuwa moja ya kombora hilo lilisafiri kwa takriban kilomita 690 .

Marekani pia ilithibitisha kwamba makombora hayo ni ya masafa mafupi.

Je kim Jong-un alisema nini?

Bwana Kim alisema kwamba ameridhishwa na mfumo huo wa kombora jipya na kudai kwamba haitakuwa rahisi kujilinda dhidi yake.

Amesema kuwa Korea Kusini haifai kufanya kosa la kupuuza onyo hilo.

Korea Kusini imeitaka Pyongyang kuwacha vitendo ambavyo havisaidii ili kupunguza hali ya wasiwasi na kusema kuwa majaribio hayo ni tishio la kijeshi.

Wizara ya mashauri ya nchi za Kigeni nchini Marekani imeitaka Korea Kaskazini kutofanya uchokozi.

Kulingana na mwanahabari wa BBC nchini Korea Kusini laura Bicker Pyongyang inailenga Korea Kusini kwa kutumia maneno na silaha.

Kombora hilo la masafa mafupi sasa linaweza kushambulia nchi yoyote ilio jirani na Pyongyang. Halafu kuna yale madai kwamba Korea kusini ni nduma kuili - ikitafuta kuleta amani mbali na kununua silaha mpya na kushiriki katika zoezi la kijeshi la pamoja na Marekani.

Matamshi hayo huenda yakazua uhasama baada ya rais wa Korea Kusini Moon Je kufanya juhudu kubwa ya kuimarisha uhusiano kati yake na rais Kim jong un.

Hata ombi la Korea Kusini kupeleka msaada wa mchele Korea Kaskazini linaonekana kukataliwa kwa sasa.

Korea kaskazini huenda inajaribu kuishawishi Korea Kusini . Pia inaonakana kuwa njia mojawapo ya kugawanya msimamo wa Washington na ule wa Korea Kusini.

Utawala wa rais Moon tayari umetaka Korea Kaskazini kuondolewa baadhi ya vikwazo ili kujenga uaminifu kati ya mataifa hayo, hatua ambayo Marekani haiwezi kufikiria.

Kwa mara nyengine tena Trump hakukosolewa katika taarifa hiyo. Hii sasa imekuwa tabia ya Pyongyang . Bwana Kim anawacha milango wazi kwa mazungumzo na rais huyo wa Marekani.

Anaonekana kutaka kujadiliana na Trump ana kwa ana na hangependelea kusema kitu ili kuharibu uhusiano wao.

Kuna muktadha gani?

Jaribio hilo ni la kwanza tangu bwana Kim na rais huyo wa Marekani Donald Trump kukutana katika eneo linalolindwa sana katikati ya mpaka wa Korea Kusini na korea Kaskazini tarehe 30 mwezi Juni.

Uzinduzi huo pia unajiri baada ya Korea kaskazini kuonyeshwa kukasirishwa kuhusu mpango huo wa zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani.

Korea Kaskazini imeonya kwamba itaathiri mazungumzo ya kuizuia Korea Kaskazini kutengeneza silaha za kinyuklia.

Takriban wanajeshi 29,000 wa Marekani wapo nchin Korea Kusini, chini ya makubaliano ya amani yalioafikiwa baada ya vita kuisha 1953.

Huwezi kusikiliza tena
The nuclear word Trump and Kim can't agree on

Mwaka uliopita , bwana Kim alisema kuwa Korea Kaskazini itasitisha majaribio ya kinyuklia na haitafanya tena majaribio yake ya makombora ya masafa marefu.

Haki miliki ya picha European Photopress Agency
Image caption Bwana Kim alizungumza na wanahabari baada ya kuikagua manowari mpya

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii