Fedha za ndani kugharamia mradi wa kufua umeme wa kilowati 2115

Uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa kufua umeme katika mto Rufiji Haki miliki ya picha IKULU TANZANIA
Image caption Raisi wa Tanzania Dokta John Magufuli akisalimiana na Waziri wa nishati wa Misri Dokta Mohamed Shaker

Raisi John Magufuli ameweka jiwe la msingi kwenye mradi mkubwa wa kufua umeme katika mto Rufiji utakaozalisha umeme wa kilowati 2115

Mradi huu utakaogharimu kiasi cha trilioni 6.5 za Tanzania, zikiwa fedha za ndani, ulipangwa kutekelezwa kwa miezi 42 hivi sasa ikiwa imebaki miezi 36 pekee ili kuukamilisha,

Umeme utakaozalishwa utasafirishwa kutoka Rufiji kuelekea Chalinze , umbali wa km 167 kisha Dar es Salaam na Dodoma pia umeme utakaozalishwa utaweza kuendesha treni za mwendo kasi.

Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Dokta Medard Kalemani amesema malengo ya serikali ni kuzalisha umeme wa megawatt 10000 ifikapo mwaka 2025.

Mradi huu una manufaa gani?

Utasaidia udhibiti uharibifu wa mazingira, Dar es Salaam pekee magunia laki 5 ya mkaa hupelekwa na kutumika kila mwezi kutoka msituni, Asilimia 71.2 ya watanzania hutumia nishati mbadala ya kuni na mkaa, ekari za mraba laki nane hukatwa kwa ajili ya matumizi ya nishati mbadala.

Mradi huu ni mkakati madhubuti wa kupambana na athari za mazingira nchini Tanzania.

Kuongeza shughuli za utalii na shughuli za umwagiliaji na pia kutoa ajira na kusaidia uimarishwaji wa shughuli nyingine za kiuchumi.

Rais Magufuli asafiri kwa Treni kwenda Rufiji

Waziri atimuliwa kazi kisa mgao wa umeme

Haki miliki ya picha IKULU TANZANIA
Image caption Rais wa Tanzania,Dokta John Magufuli

Mradi huu unajengwa na wakandarasi kutoka makampuni makubwa mawili kutoka Jamuhuri ya kiarabu ya Misri ikishirikiana na Kampuni ya Tanzania ya usambazaji umeme, Tanesco.

Rais wa Tanzania, Dokta John Magufuli amesema kuwa mradi huu ni utekelezaji wa ndoto ya baba wa taifa mwalimu nyerere miaka ya 70 baada ya kutambua kuwa nishati ya umeme ni kichocheo cha maendeleo ya sekta zote.

''Kupitia mradhi huu nchi yetu imeudhihirishia ulimwengu kuwa sisi ni taifa huru linaloweza kujiamulia mambo yake kwa kuzingatia vipengele vyake,nyote mnafahamu mradi huu ulikabiliwa na vikwazo vikali kutoka ndani na nje ya nchi yetu , upinzani huo ulianza baada ya kutangazwa kwa azma ya kuanza mradhi huu mwezi Juni mwaka 2017.''

Mada zinazohusiana