Gareth Bale: Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales kuhamia ligi ya China

Gareth Bale Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gareth Bale

Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales ,Gareth Bale anajiandaa kujiunga klabu ya China ya Jiangsu Suning kwa mkataba wa miaka mitatu.

Watu walio na uhusiano wa karibu na mchezaji huyo raia wa Wales aliyevunja rekodi ya ufungaji mabao wamethibitisha ripoti hizo nchini Uhispania mpango hjuo haujakamilika reports in Spain that although Bale yuko ''karibu sana'' kuondoka.

Meneja wa Real Zinedine Zidanealiwahi kusema kuwa Bale, 30, ''anakaribia kuondoka'' bada ya kumuacha nje ya kikosi kilichochuana na Bayern Munich katika mechi ya kabla ya kuanza kwa msimu abapo walifungwa mabao 3-1.

Zidane aliongeza kuwa kuondoka kwake "kutakuwa na na manufaa kwa kila mtu".

Ripoti zinaarifu kuwa uhamisho wa Bale kwenda China utamwezesha kulipwa euro milioni moja kwa wiki.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gareth Bale alijiunga na Real Madrid mwaka 2013

Bale alijiunga na klabu hiyo ya Uhispania mwaka 2013 katika uhamisho uliovunja rekodi wa euro milioni 85 kutoka Tottenham.

Amesalia na mkataba wa miaka mitatu katika klabu hiyo ya Bernabeu ambako alishinda mataji manne ya Champions League, moja ya La Liga title, Copa del Rey, mataji matatu ya Uefa Super Cup na Kombe l Dunia la vilabu mara tatu.

Bale aliifungia Real mabao matatu pamoja na mkuju wa penalti katika finali nne za Champions League waliponyakua ushindi mwaka 2014, 2016, 2017 na2018.

Aliichezea Real Madrid mechi 42 msimu uliopita na wakati mwingine alizomewa na mashabiki wa nyumbani wakati wa mechi za La Liga

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bao la kusisismua la Bale iliisaidia Real Madrid kuifunga Liverpool katika fainali ya Champions League 2018

Kurejea Real kwa Zidane kama kocha wa klabu hiyo mwezi Machi kumeelezewa kuwa "habari mbaya" na ajenti wa mshambuliaji huyo, Jonathan Barnett, kwa sababu Zidane hakutaka kufanya kazi na Bale na kwamba wawili hao walitofautiana kuhusu mtindo wa mchezo

Bale alimaliza msimu uliopita akiwa kwenye benchi na kushuhudia timu yake ikipewa kipigo kikali kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 20.

Walishindwa mara 12 na kumaliza ligi katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 68 ikiwa ni alama 19 nyuma ya mabingwa Barcelona.

Real pia iliondolewa katika kinyang'anyiro cha kuwania Champions League na Ajax.

Wachezaji wengine wa zamani wa ligi ya Premia waliohamia China, ni Marko Arnautovic, Marouane Fellaini, Mousa Dembele na Oscar.

Bale akikamilisha mshakato wa uhamisho wake kwenda Jiangsu, ataungana na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Italia Eder na kiungo wa kati wa Brazil Alex Teixeira, ambaye alipigiwa upatu kujiunga na Liverpool mwaka 2016 kabla ahamie China.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii