New Zealand: Mwanamume aliyemshika mvulana nyeti zake afutiwa mashtaka

Child wrapped in a towel

Mwanamume wa miaka 79 raia wa China alifikishwa mbele ya mahakama moja nchini New Zealand kwa kumshika sehemu za siri za mtoto wa kiume katika chumba cha kubadilisha nguo baada ya kuogelea.

Lakini mtu huyo aliponea shtaka la unyanyasaji wa kingono licha ya kukiri kuwa alifanya kitendo hicho .

Jaji alikubaliana na hoja ya mshukiwa kuwa tabia hiyo ni sehemu ya utamaduni wa Wachina unaosharia upendo, vyombo vya habari vimeripoti.

Kuna ukweli wowote katika 'utamaduni' huo na China inalizingumzia vipi suala hili?

Kilichotokea wakati wa kisa hicho?

Mwaka jana mwezi Agosti katika kituo cha kujiburudisha mjini Christchurch, mwanamume wa Kichina anayefahamika kama Ren Changfu alimuona mtoto mvulana akibadilisha nguo zake baada ya kuogelea na bila kufahamu kuwa mtoto huyo alkuwa na baba yake, Ren alimsogelea na kuanza kusema na nae huku akishika na kuchezae uume wa mtoto huyo huku akicheka na kuzishika tena, Vyombo vya habari vya New Zealand viliripoti.

Baba yake mtoto huyo alimuomba aachane nae la sivyo atapiga simu polisi na kumripoti kw autovu wa nidhamu.

Mwanamume huyo ambaye alihamia New Zealand mwaka 2009, aliwambia maafisa waliokuja kumkamata kuwa hakujua kitendo chake ni makosa na kuongeza kuwa mtoto huyo alimkumbusha mjukuu wake aliyepo China ambaye anampenda sana.

Binti ya Ren alitayarisha ripoti iliyosema kuwa nchini China kumshika mtoto wa kiume sehemu zake za siri na kuzichezea ni ishara ya kuonesha upendo.

Jaji wa mahakama ya wilaya ya Christchurch, Alistair Garland alikubaliana na utetezi wake na kuamua kuwa Ren hakua na nia ya kumdhulumu kimapenzi mtoto huyo.

Aidha jaji alisema kuwa Ren ameshutuka sana kujua kuwa aliwakwaza vibaya wazazi wa mvulana huyo na kwamba "yuko tayari kufanya lolote ili asamehewe", na kuongeza kuw kosa hilo linastahili kueleweka kwa misingi ya utamaduni wajamii ya Bw. Ren".

Wazazi wa mtoto huyo wamekubali kumsamehe na pamoja na dola 670 alizolipa kufidia kosa lake.

Wachina wenyewe waanasema nini?

Kisa hicho kilizua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii kote nchini China kwa zaidi ya wiki moja,baadhi ya watu wakisema kuwa alitafsiri vibaya utamaduni wa jamii yao.

Watu 300 kati ya 1200 waliojadili suala walihisi kuwa kitendo chake hakihusiani kwa vyovyote na utamnaduni wao.

Wengine karibu 200 walisema washawahi kusikia utamaduni kama huo lakini wanasema ni utamaduni uliopitwa na wakati japo bado unatumika miongoni mwa watu wanaoishi vijijini.

Maelezo ya picha,

Jamii ya wachina inamthamini sana mtoto wa kiume

Waliosalia walikuwa wakiuliza maswali huku wengine wakilaani kitendo hicho.

Familia nyingi za Kichina kwa muda mrefu zimedhamini mtoto wa kiume kuliko wa kike.

Kumgusa mtoto wa kiume nyeti zake ni njia moja ya kuimarisha fahari ya familia yake.

Kabla nepi za kuwasunga watoto kupata umaarufu watoto wa kiume walikuwa wakivishwa suruale ambayo ilikuwa wazi upande wachini na ilikuwa ikionesha korodani zake.

Lakini walioruhusiwa kuzigusa ni wazee na watu wa karibu na wazazi wake. Mtu mwingine yeyote akigusa sehemu nyeti ya mtoto wa kiume ambaye hana uhusiano na watu wake alichukuliwa hatua kali.

Kumeshuhudiwa visa kadhaa kama alivyofanya Bw. Ren Uchina kwenyewe:

  • Mwezi Machi mwaka huu mwanamume mmoja alishtakiwa kwa kugusa hadharani sehemu nyeti za mtoto wa kiume asiyemjua huku akimtania.Aliishia kulipa fidia ya Yuan 150,000.(£17,550; $21,800)
  • Mwaka 2015, Mama mmoja mstaafu na mjikuu wake wa kiume walikuwa wakitembea njiani wakapatana na mzeewasiye mjua na bila tahadhari mzee huyo alianza kushika sehemu za siri mtoto huyo. Bibi yake alimzuia mzaee huyo kuendelea na tabia hiyo, kwa mijibu wa Gazeti la kitaifa la PeopleDaily

Wakili Xue Yuhai alinukuliwa na Gazeti hilo akitoa wito kwa wazazi kupiga ripoti polisi wakishuhudia kitu kama hicho.

Prof Liu Wenli wa Chuo Kikuu cha Beijing na mtaalamu wa jinsi ya kuwafunza watoto jinsia zao anasema kuwagusa wavulana nyeti zao ni utamaduni ''uliooza'' na kuongeza kuwa watu wazima hawajui jinsi ya kuwaheshimu watoto wao.

Japo watoto wanajua haki zao na jinsi ya kujikinga na watu kama hao bado wazazi wao wanakubaliana na utamaduni huo hususan katika baadhi ya miji, alisema Prof Liu.

Anasema kumgusa mtoto uchi wake kunaweza kumfanya afikirie ni jambo la kawaida haliambayo inaweza kuwaweka katika hatari ya kudhulumiwa kimapenzi.

Wazazi wanatakiwa kuwafahamisha watoto wao kuwa nyeti zao zinastahili kuguswa na wazazi wao wakati wakiwaogesha au daktari wakati akiwafanyia uchunguzi wa kimatibabu, Prof Liu alipendekeza.