Spika Nancy Pelosi asema matamshi ya 'panya waliojaa' dhidi ya mbunge mweusi ni ya kibaguzi

Elijah Cummings, mbunge wa a Democratic Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bwana Trump aliitaja wilaya ya vbaltimnore ya bwana Cummings kama iliojawa na panya wengi.

Spika wa chama cha Democrats nchini Marekani Nancy pelosi amemshutumu rais Donald Trump kwa kuishambulia wilaya ya Baltimore yenye wakaazi wengi weusi kuwa eneo lililojaa panya wengi.

Bwana Trump alimshambulia mbunge Elijah Cummings na wilaya yake ya Maryland katika mtandao wa twitter.

Rais huyo alitaja wilaya ya bwana Cummings yenye raia wengi weusi - Baltimore kama iliovamiwa na panya.

Bwana Cummings ni 'mnyanyasaji', bwana Trump aliandika akikosoa jinsi wahamiaji waliopo katika mpaka wa Marekani na Mexico walivyopata shida.

Kama mwenyekiti wa kamati ya uangalizi , bwana Cummings amechochea uchunguzi mwingi kufanywa kuhusu sera za utawala wa rais Trump , ikiwemo jinsi ilivyowaadhibu wahamiaji katika vituo vya kuwazuia.

Bi Pelosi aliwaongoza wabunge wa Democrats katika kumtetea bwana Cummings akiyashutumu machapisho ya Trump katika mtandao wake wa twitter.

Machapisho yaliondikwa dhidi ya Cummings ambaye asilimia 50 ya wakaazi wa wilaya yake ni weusi kulingana na data ya idadi ya watu nchini Marekani.

Matamshi ya rais Trump yanajiri wiki chache tu baada ya kukosolewa kwa chapisho jingine la twitter akiwaambia wanawake wa chama cha Congress kurudi wanakotoka.

Ujumbe huo uliwalenga wabunge weusi akiwemo Alexandria Ocasio-Cotez, Rashida Tlaib, Ayanna Pressley na Ilhan Omar - wote wakiwa raia wa Marekani.

Ni nini kilichosababisha chapisho hilo la bwana Trump?

Wiki iliopita bwana Cummings alimshutumu kaimu katibu wa usalama Kevin McAleenan na hali ilivyo katika vituo vya mipakani katika mkutano mmoja wa bunge.

Katika majibizano bwana McAleenan , bwana Cumminga alitaka hali kuimarishwa katika vituo hivyo.

Bwana Cummings ambaye anawakilisha wilaya ya Maryland , alisema kwamba utawala wa Trump hauna huruma katika kuwakabili wahamiaji .

Akichapisha katika twitter siku ya Jumapili bwana Trump alionekana kukasirisha na matamshi ya Cummings.

Ujumbe huo wa twitter unajiri siku chache tu baada ya kamati ya Democrats kutaka kujua mawasiliano ya kisiri ya maafisa wandamizi wa ikulu ya Whitehouse.

Bwana Cummings aliushutumu utawala wa Trump kwa kutoweka rekodi za mawasiliano yake kulingana na sheria.

Kamati hiyo ya uchunguzi ni miongoni mwa kadhaa zinazofuatliwa na bunge la Democrats kwa rais huyo na utawala wake.

Je machapisho ya Trump yamejibiwa vipi?

Akiwa mkosoaji mkubwa wa bwana Trump , bwana Cummings amemjibu akisema ni haki yangu ya kikatiba kuufanyia uangalizi uongozi wako.

Na pia ni jukumu langu la kuwapigania watu wungu.

Katika ujumbe mwengine wa twitter Meya wa Baltimore jack Young alimtaja bwana Trump kuwa masikitiko makubwa kwa raia wa mji wake, taifa lote na ulimwengu mzima kwa jumla

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nancy Pelosi amemshutumu bwana Trump kwa kuchapisha ujumbe wa kibaguzi katika twitter

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii