Van filled with drugs crashes into police car
Huwezi kusikiliza tena

Gari lililobeba mihadarati yenye thamani ya $140m kwa siri lagonga gari la polisi mjini Sydney

Mshukiwa mmoja ambaye amekuwa akisafirisha mihadarati kutoka eneo moja hadi jing nchini Australia amekamatwa baada ya gari lake lililokuwa na mihadarati yenye thamani ya $200m kugonga gari la polisi wa kupiga doria ambalo li;likua limeegeshwa kandokando ya barabara mjini Sydney.

Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 28 aligonga gari hilo la polisi kwa kasi , na kuvunja eneo lake la mbele kabla ya kutoroka.

Hatahivyo maafisa wa polisi walimkamata saa moja baadaye katika eneo la Eastwood , kijiji kimoja kilichopo kaskazini mwa mji huo.