Ngono ya lazima: Mwanamke anapomlazimisha mwanamume kushiriki ngono , je huo ni ubakaji?

Pingu Haki miliki ya picha Getty Images

Wakati mwanamume anapofanya tendo la ngono na mwanamke bila ruhusa yake ,huo ni ubakaji. Lakini je inakuwaje wakati mwanamke anapomlazimu mwanamume kushiriki ngono naye bila ruhusa yake?

Huo sio ubakaji chini ya sheria za Uingereza na Wales lakini mwanzilishi wa utafiti mpya kuhusu swala hilo pengine anasema unafaa kuwa ubakaji.

Baadhi ya wasomi watakerwa ba habari hii

Dkt Siobhan Weare wa chuo kikuu cha sheria cha Lancaster alifanya utafiti wa kwanza kuhusu mwanamume kulazimishwa kushiriki tendo la ngono mwaka 2016-7 na kukusanya habari kutoka kwa zaidi ya wanaume 200 kupitia utafiti uliofanyika kupitia mitandao.

Utafiti wake wa hivi karibuni uliochapishwa wiki hii kutokana na mahojiano ya ana kwa ana na wanaume 30 kati ya mwezi Mei 2018 hadi Julai 2019-unaonyesha kwa maelezo ya ndani jinsi ngono ya lazima inapofanyika, madhara yake pamoja na sheria inavyosema.

Wote walioshiriki hawakutajwa majina lakini nitamuita mmoja wao kwa jina John. John anasema kwamba ishara ya kwanza kwamba mambo hayakua shwari ni wakati mwenzake alipoanza kujiumiza .

Baada ya kisa cha kutisha alimkimbiza kwa matibabu. Wapenzi hao wawili walijadiliana kuhusu uwezekano wa sababu za kisaikolojia.

Takriban miezi sita baadaye badala ya kujiumiza mwenyewe alimlenga John.

''Nilikuwa nimeketi sebuleni na alikuja kutoka jikoni , na kunipiga ngumi kwa nguvu katika pua yangu na kukimbia akicheka'', John anasema. Ugomvi ukaanza polepole na kuendelea mara kwa mara.

Alijaribu kupata usaidizi kutoka kwa GP, John anasema. Alipatiwa ushauri nasaha na kuambiwa amuone dkt wa saikolojia . Hatahivyo hakwenda.

''Angeweza kuja nyumbani kutoka kazini na kutaka kushiriki ngono kwa nguvu'', anasema. ''Yeye angetumia nguvu na ikafikia wakati ambapo nilikuwa nikichukia anaporudi kutoka kazini''.

Wakati mmoja John aliamka na kugundua kwamba mpenzi wake alimfunga kamba mkono wake wa kulia na kitanda. Na baadaye akaanza kumgonga katika kichwa na spika kubwa akamfunga mkono mwengine na kitanda na kujaribu kumlazimisha kushiriki ngono naye.

Akiogopa mamumivu aliokuwa nayo John alilazimika kufanya anachotaka - baadaye alimpiga tena na kumwacha amefungwa kwenye kitanda kwa nusu saa kabla ya kurudi na kumfungua.

Baadaye alikataa kuzungumzia yaliojiri. Muda mfupi baada ya visa hivyo akapata ujauzito na mgogoro aliokuwa nao ukapungua.

Lakini miezi michache baada ya mtoto kuzaliwa ,John aliamka usiku mmoja na akajipata kwamba mpenzi wake amemfunga mkono wake wa kulia katika kitanda.

Baadaye anasema mpenzi wake akamlazimisha kula dawa ya Viagra. hakuna kitu ningeweza kufanya , anasema.

Baadaye nilienda kuoga sijui kwa dakika ngapi ....nilishuka chini. Kitu cha kwanza alichoniuliza wakati nilipoingia katika chumbani ni tutakula nini jioni?

Wakati John anapoanza kuwaambia watu kuhusu kisa hicho anasema kwamba wanashangaa.

''Nimekuwa nikiulizwa ni kwa nini niliondoka nyumbani? Ndio ni nyumba yangu ambayo niliwanunulia watoto wangu''.

Madai ya habari ya John yamerejelewa katika baadhi ya visa vya wanaume wengine ambao Dkt Weare aliwahoji.

Mojawapo ya mambo aliyogundua ni kwamba mshukiwa katika uingiliaji wa lazima ni mwanamke .

Utafiti wake unaangazia uingiliaji wa lazima miongoni mwa wanaume na wanawake na kwamba visa hivyo huwa moajwapo ya sababu za migogoro nyumbani.

Tatizo la watu kutomuamini mwanamume anapozungumza kuhusu vitendo kama hivyo pia vilitajwa na baadhi ya waliohojiwa.

''Ungefurahia ama umeripoiti mapema sana'', mwanamume mmoja aliambiwa na afisa wa polisi.

Mshiriki mwengine alisema: Tunaogopa kuzungumzia na tunapozungumzia hatuaminiki kwa kuwa sisi ni wanaume.

Ni vipi mwanamume anaweza kudhulumiwa kwa njia hiyo? mwangalie ni mwanamume."

Kitu kimoja ambacho utafiti wa Weare unapinga ni kwamba tendo la ngono kwa lazima haliwezekani kwa kuwa wanaume wana nguvu ukilinganisha na wanaume.

Chengine ni kwamba wanaume hulitazama tendo la ngono na wanawake kama fursa kubwa.

Weare anasema kwamba msisimuko wa mwili wa mwanamume hutokana na kichocheo.

Anasema kwamba wanaume wanaweza kupata msisimuko wa mwili na kusalia nao hata iwapo wamekasirika ama ni waoga.

Pia kuna utafiti unaosema kwamba wanawake wanaweza kusisimka wakati wanapobakwa kwa kuwa mili yao husisimka kimaungo.

Hili ni swala la waathiriwa wanaume na wanawake ambalo huwa halijadiliwi vya kutosha lakini kuna ushahidi kulihusu.

Mmoja ya waliohojia katika utafiti huu mpya alielezea kwamba walienda nyumbani na mwanamke baada ya ya kutoka katika klabu ya burudani na kulala baada ya kupewa dawa.

Anasema kwamba baadaye alilazimishwa kushiriki katika tendo la ngono bila ya yeye kujua


Weare anasema kwamba wengi wa wale walioshiriki katika utafiti huo mpya walidai kwamba visa vya wao kulazimishwa na wanawake kushiriki tendo la ngono vilikuwa ubakaj na kwamba wengine walikasirishwa na swala kwamba huenda sio ubakaji chini ya sheria za Uingereza na Wales.

Kuna mafadhaisho kwamba jamii ya Uingereza huenda wasiijumuishe kama ubakaji.