Kifyatua kombora chanaswa kwenye ndege katika begi la usafiri

Kifaa cha kurushia kombora Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanaume huyo amesema kifaa hicho ni zawad kutoka kuwait

Maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege nchini Marekani wamekamata kifaa kinachorushia kombora, kikiwa kwenye mzigo wa abiria mjini Maryland.

Chombo hicho kiligundulika kwenye mzigo wa mwanaume mmoja ambaye alisema alikuwa akifanya kazi kwenye jeshi.

Aliwaamba maafisa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baltimore/Washington kuwa kifaa hicho kilikuwa zawadi kutoka Kuwait.

Kifaa hicho kimechukuliwa na maafisa wa zima moto kwa ajili ya kukiteketeza.

Idara ya usalama wa usafirishaji imesema katika taarifa yao kuwa ''mwanaume huyo mkazi wa Jacksonville, Texas, aliwaambia maafisa kuwa alikuwa mfanyakazi wa jeshi mwenye bidii''.

Taarifa iliongeza: ''Bahati, kifaa hicho hakikuwa kikifanya kazi. kilishikiliwa na kupewa kwa maafisa wa zima moto kwa ajili ya kukiteketeza. Mtu huyo aliruhusiwa kuendelea na safari.''

Silaha za kijeshi hazipaswi kubebwa kwenye mabegi.

Si mara ya kwanza kwa mamlaka kukutana na matukio ya namna hiyo. Mwezi Agosti mwaka 2018, maafisa waligundua vifaa mithili ya guruneti kwenye begi katika uwaja wa ndege wa kimataifa wa Newark Liberty.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii