Madai ya ubakaji: Kesi ya Neymar yatupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi

Neymar Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Neymar amekana shutuma dhidi yake

Polisi wanaochunguza madai ya ubakaji dhidi ya mchezaji wa Brazil Neymar wamesema wametupilia mbali kesi hiyo.

Ofisi ya mwanasheria wa São Paulo imesema kesi hiyo imetupiliwa mbali kutokana na kukosekana ushahidi, lakini suala hilo litapelekwa kwa waendesha mashtaka kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.

Uchunguzi ulianza baada ya mwanamitindo Najila Trindade alidai kuwa mchezaji huyo alimshambulia katika hoteli jijini Paris, Ufaransa, mwezi Mei.

Neymar amekana shutuma dhidi yake akidai kuwa amekuwa akifanyiwa hila.

Msemaji wa Neymar ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kuwa hakuwa tayari kuongelea uamuzi wa polisi.

Haki miliki ya picha AFP

Kesi hiyo ilitawala vichwa vya habari vya magazeti ya nchini Brazil.

PSG: Neymar anaweza kuondoka

Neymar asusia mazoezi PSG - kunani?

Suala hilo kwa mara ya kwanza lilijulikana mwezi Juni, baada ya nyota huyo wa Paris St-Germain kuchapisha video ya dakika saba kwenye ukurasa wa Instagram ikiweka wazi kuwa anahusishwa na tuhuma za ubakaji. Pia alichapisha ujumbe wa Whatsapp na picha zinazodaiwa kuwa za mwanamke anayemshutumu.

Katika video, anasema alilazimika kuweka hadharani ''kuthibitisha kuwa hakuna kilichotokea''.

Bi Trindade kisha akajitokeza hadharani kwenye mahojiano ya televisheni na kutoa picha na video fupi iliyoonyesha wawili hao wakizozana.

Polisi baadae walifungua kesi ya udhalilishaji dhidi ya bi Trindade.

Mwanamitindo huyo pia aliachwa na wanasheria kadhaa.

Waendesha mashtaka sasa wana siku 15 za kutathimini kesi kabla jaji hajatoa uamuzi wa mwisho.

Tuhuma

Bi Trindade ambaye pia ni raia wa Brazil alisema kuwa alikutana na Neymar katika mtandao wa Instagram.

Alikiambia chombo cha habari cha Brasil cha SBT kwamba alivutiwa na mchezaji huyo wa Brazil na alitaka kushiriki ngono naye.

Amasema kwamba alisafirishwa kutoka Paris na kulipiwa hoteli na mchezaji huyo.

Kilichokuwa kwenye video

Kanda ya Video inaonyesha mtafaruku kati ya bi Trindade katika chumba kimoja cha hoteli-ikidaiwa kuchukuliwa na bi Trindade.

Wawili hao wanaonekana wakiwa wamelala katika kitanda ambapo baadaye mwanamke huyo anasimama na kuanza kumpiga mwanamume aliyelala kitandani ambaye anajikinga na miguu yake.

Mwanamke huyo anasema nitakupiga, unajua kwa nini kwasababu umenipiga , mtafaruku huo ukionekana kuwa mkutano wao wa pili .

Neymar amesema kuwa yeye na bi Trindade walikutana mara mbili.

Katika mahojiano hayo ya Runinga ya SBT , Bi Trindade alisema kuwa alianza kuelewa kila kitu kilichofanyika baada ya mkutano wao wa kwanza ulipokamilika na kwamba alirudi ili kuthibitisha kitendo kilichofanyika huku akitaka haki kufanyika.

Kanda hiyo ya Video ilionyeshwa katika kituo hicho cha Brazil.

Mada zinazohusiana