Wanawake waamua kuchora nyuso zao kwa damu ya hedhi

A woman uses water mixed with menstrual blood to water plants Haki miliki ya picha Renata Chebel para DanzaMedicina
Image caption Kupanda mwezi ni utamaduni wenye misingi tamaduni za wahenga ambazo zilichukulia damu ya hedhi kama ishara ya uwezo wa kuzaa, wanasema wanaotekeleza utamaduni

Kila mwezi, Laura Teixeira hufanya mila ya "kuhusiana " na dunia.

Akiwa na umri wa miaka 27-hukusanya damu yake ya mwezi, kuipaka usoni na kuiichanganya nyingine iliyobaki na maji , ambayo humwagilia mimea.

Utaratibu huu unaitwa "kupanda mbegu ya mwezi ",unafuatwa kutokana na tamaduni za mababu ambao walisherehekea damu ya mwezi na kuitambua kama ishara ya uzazi.

Wanawake wanaofuata utamaduni huu wana namna yao ya kushereheke "miezi ", yao, ambayo waliona kama ilikuwa na awamu na mizunguko kila mmoja ukiwa na maana yake.

Laura ameiambia BBC kwamba alikuwa na maneno maalum ya kumwagilia mimea: "Samahani, nisamehe , Ninakupenda na Ninakushukuru", alirudia rudia maneno haya. "Nilikuwa na picha ya mimea ikiota na kuwa mizuri na kupokea virutubisho vingi ," anasema.

lakini alipofuta damu ya mwezi kwenye mwili wake, alisema alifunga tu macho yake na kuhisi kuwa mwenye shukrani na mwenye nguvu tena.

'Nguvu sana'

Kwa Laura, mila hii ni juu ya kuwaongezea nguvu wanawake.

"Moja ya ubaguzi mkubwa kabisa ni mtizamo hasi wa jamii juu ya damu ya mwezi na jinsi ambavyo wanawake bado wanahisi aibu kuhusu hedhi yao," anasema.

Haki miliki ya picha Laura Mocellin Teixeira
Image caption Laura pia hiuchora uso wake na kifua kwa damu ya hedhi

Kupanda mwezi ni''kitu rahisi sana , lakini chenye nguvu nyingi, kinachoponya, na zoezi la kina kwa mwanamke ," kwa mujibu wa Morena Cardoso, mwanasaikolojia , mchezaji densi na mwandishi dancer aliyeanzisha kampuni inayotekeleza mila hiyo -World Seed Your Moon Day mwaka 2018.

Mwaka jana iliwavutia watu 2,000 waliopanda mbegu za damu yao ya hedhi kwa pamoja katika maeneo ya umma.

Wazo la tukio hilo, anasema Morena, ni kwamba "damu ya hedhi , kama ilivyo kwa mwanamke , sio sababu ya aibu , bali ni ya kujivunia na ni nguvu ".

Tarehe ijayo ni 4 Augusti.

'Kazi ya kiroho ya wanawake'

Kwa mujibu wa Morena, miongoni mwa tamaduni za wazawa katika Amerika Kaskazini (mkiwemo Mexico), na Peru, damu ya hedhi ilikuwa inamwagwa kwenye ardhi kuifanya iwe yenye rutuba na yenye kumea mimea kwa wingi.

Iliwakilisha muda wa ushirika na kazi ya kiroho ya wanawake, na ibada ya wanawake wanaojiandaa sasa kuwa na heshima ya kuwa wanawake.

Haki miliki ya picha Ana Oliveira
Image caption Mwaka jana iliwavutia watu 2,000 waliopanda mbegu za damu yao ya hedhi kwa pamoja katika maeneo ya umma

Lakini katika jamii nyingine kuna "mitazamo hasi " ya damu ya hedhi, anasema Daniela Tonelli Manica, mtaalam wa historia ya Binadamu katika Chuo Kikuu cha Brazil Unicampambaye amefanyia uytafi utafiti suala la hedhi miongoni mwa jamii kwa miaka 20.

"Damu ya hedhi huangaliwa kama utokwaji wa damu usio na maana ," anasema, "ambao huwekwa katika kundi moja na kinyesi na mkojo - kitu ambacho unamalizana nacho msalani , ambacho hakipaswi kuonekana machoni pa watu."

katika miaka ya 1960s, vuguvugu la haki za wanawake lilitaka kubadilisha mitazamo hii , likiwataka wanawake kuzungumzi zaidi juu ya miili yao na kuheshimu maumbile yao.

Wasanii walikuja baadae kuvumbua ishara ya damu ya hedhi kuelezea maoni yao ya kisiasa kuhusu masuala ya mazingira, ngono na jinsia.

''Tumbo kubwa la uzazi''

Haki miliki ya picha Sofia Ribeiro
Image caption Renata anasema kwamba ''kupanda mbegu ya mwezi'' yameufanya mtazamo wake kwa dunia kuwa kama "tumbo kubwa la uzazi" linaloota

"Nilidhani ilikuw ani haki na jambo sahihi kurejesha kwa dunia kile inachutupatia ."

Hukusanya damu yake ya hedhi bafuni na kuimwagilia kwenye mimea ya maua ya basil aliyoipanda kando ya nyumba yake kwenye vyungu.

Renata pia hupanda mimea ya minti ambayo haimwagilii na damu yake ya hedhi na inaonekana kuwa "dhaifu ". anatani kuwa ina "utapiamlo".

Mara ya kwanza Renata mwenye umri wa miaka 43-alipopata hedhi , akiwa na miaka kumi na zaidi, alikuwa ameambiwa kuwa : "Sasa wewe ni mwanamke mchanga, utaanza kuvuja damu kila mwezi na hakuna mtu anahitaji kufahamu hilo ".

Aliiona hedhi yake kama "maudhi " ya mara kwa mara na aliwaonea wivu wanaume ambao hawakukuumbwa kupitia hedhi .Lakini sasa anaiona hedhi yake kama kitu "kitakatifu".

Mwiko

Utafiti wa dunia waliofanyiwa wanawake 1,500 walio na umri kati ya miaka 14 na 24 unaonyesha kwa kiwango gani suala la hedhi bado ni mwiko katika jamii nyingi.

Kwa mujibu wa utafiti - ulioagizwa na Johnson & Johnson na kufanyika katika nchi za Brazil, India, Afrika Kusini, Argentina, na Ufilipino - wanawake wanahisi aibu wanapoazima sodo(vitamba vya hedhi), wanaoonekana wakizihifadhi baada ya kuzitumia na hata kusimama kutoka kwenye viti vyao wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.

Haki miliki ya picha Mel Melissa para DanzaMedicina
Image caption Bado suala la hedhi bado ni taboo miongoni mwa jamii mbali mbali duniani

''Utata''

Lakini si kila mmoja yuko tayari kukubali mila ya kupanda mbegu ya mwezi -na hivyo ndivyo Laura alivyoibua mjadala mwezi Juni baada ya kutuma picha ya selfie iliyoonyesha uso wake na kifua vilivyopakwa damu ya hedhi.

"Nilikuw ana wafuasi 300na nilifikiria utakuwa tu kama ujumbe wa kawaida nilioutuma kwenye ukurasa wangu wa mtandao wa kijamii ili kumsaidia mwanamke mwingine kuelewamada," alisema.

Haki miliki ya picha Morena Cardoso
Image caption Morena Cardosoanaamini kuwa mada ya hedhi ya wanawake inapaswa "rahisi na ya kueleweka"

Siku nne baadae , alibaini kuwa alikuwa amedhalilishwa kwenye Instragram ambapo vibonzo vya akaunti ya Instagram vilitumiwa kumkejeli .

Mchekeshaji mwenye utata nchini Brazil, Danilo Gentili, alifikiri kuwa lilikuwa jambo la maana kutuma picha kwa wafuasi wake wa Instagram milioni 17 , akisema : "damu ya hedhi ni ya kawaida ; kitu ambacho hakikuwa cha kawaida ni kuipaka kwenye uso wako ".

Huwezi kusikiliza tena
Wasichana wa Turkana hukosa masomo wakati wa hedhi

Lakini utani wake haikuwafurahisha wengi - majibu 2,300 , mengi yakiwa ni ya wale walioonyesha kutofurahishwa nao.

Laura anasema kuwa yaliyotokea kuhusu ujumbe wake wa picha yanathibitisha tu jinsi suala la hedhi lilivyo mwiko.

"Watu wanafikiri kwamba ikiwa kama kitu si cha kawaida kwao, basi lazima kisikubalike. Wanafikiri wanaweza kujificha nyuma ya simu zao za mkononi na kutumia maneno ya chuki tkumuumiza mtu fulani," anasema.

"Haya ni majimaji ya mwili wangu na ninaamua ni nini cha kawaida au si cha kawaida, ili mradi siingilii maisha ya mtu yoyote."

Laura anasema "Jambo lisilo la kawaida ni kuwapaka watu wengine. Nitaacha kujipaka damu yangu ya hedhi siku ile tu tutakapoona kuwa damu ya hedhi ni kitu cha maumbile , na si cha kawaida ."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii