Nahodha wa Meli ya Iran iliyotekwa ashutumu kikosi cha majini cha Uingereza

Grace 1
Image caption Grace 1

Nahodha wa meli ya mafuta iliyotekwa na iliyokuwa imebeba mafuta ya Iran amesema kuwa kikosi cha majini cha Uingereza kilitumia "kikosi cha ghasia " katika kuiteka meli.

Mapema wiki hii, vikosi vya Marekani viliwalazimisha maafisa wa Gibraltar ambao meli yao ya mafuta ilikuwa imebeba mafuta kuelekea nchini Syria jambo ambalo lilikuwa ni ukiukaji wa vikwazo vya Muungano wa Ulaya.

Nahodha amesema kuwa kikosi cha wanamaji cha Uingereza waliwalazimisha wahudumu wake ambao hawakuwa na silaha kupiga magoti kwa kuonyeshwa mtutu wa bunduki.

Hata hivyo Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema kuwa kutekwa kwa meli hiyo ilikuwa ni kulingana na "sheria na miiko ya kimataifa".

Tarehe 4 Julai, takriban wanamaji 30 kutoka kikosi cha askari wa uvamizi 42 walisafirishwa kwa ndege kuutoka nchini Uingereza hadi Gibraltar kusaidia kuikamata meli na shehena yake , kufuatia ombi la serikali ya Gibraltar.

Nahodha wa chombo hicho cha majini, raia wa India ambaye ameomba jina lake lisitajwe amesema kuwa alisema kuwa aliamrishwa na polisi kuingia ndani ya meli na kushusha ngazi ya meli yake.

Lakini kabla ya mtu yeyote kuingia , helikota ya kijeshi ilitua ndani ya meli katika " hatua ambayo ilikuwa ni ya hatari sana", amesema.

Aliiambia BBC kuwa alijitambulisha kama nahodha, lakini kikosi cha wanamaji kilimpuuza na badala yake kikamnyooshea mtutu wa bunduki na kumuambia kwa sauti kali "angalia mbele, angalia mbele ".

Amesema : "Hawakujali kama nilikuwa wa maana … hapakuwa na sheria … tulikuwa na wahudumu 28 ambao hawakua na silaha. Nilikuwa katika hali ya mshtuko , kila mtu alikuwa katika hali ya mshtuko .

"Unawezaje kuingia kwenye meli kama hivi na kikosi chenye silaha kikosi chenye ukatili. Kwa sababu gani ?"

Amesema kuwa kikosi cha wanamaji cha Iran kingeweza kuingia ndani ya meli na kumwambia tu kwamba amekamatwa.

Nahodha alikubali kuzungumza na BBC kwa masharti kuwa jina lake halitatumiwa, akisema kuwa yeye na wahudumu wameshauriwa na maafisa wa ubalozi wa India kutotambulika majina yao huku mchakato wa kisheria ukiendelea.

Haki miliki ya picha MINISTRY OF DEFENCE
Image caption Vikosi vya majini vya Uingereza Royal Marines - vilitua ndani ya helikopta yao katika meli ya Grace 1

Alipoulizwa ikiwa alihisi kuwa kulikuwa na ukiukaji wowote wa sheria wa meli yake au mizigo , nahodha huyo alisema kuwa "alifuata taratibu za kampuni", na kuongeza kuwa hakujua kuhusu vikwazo vya Muungano wa Ulaya dhidi ya Syria.

Tangu wakati huo nahodha huyo alikamatwa na kulipiwa dhamana na mamlaka za Gibraltar.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema operesheni ya kwanza ya meli ya Grace 1 ilikuwa "ya kawaida " na kwamba vikosi vya Uingereza vilivyokuwa na silaha "viliiteka kwa viwango vya juu vya kikazi ".

Polisi wa kikosi cha majini cha Gibraltar Royal - Gibraltar walisema kuwa wanajeshi waliiingilia kati kwa usaidizi wa maafisa wao na walitumia "kiwango cha chini cha nguvu " kuhakikisha maafisa wangeweza kuingia ndani ya meli, kuwashughulikia wahudumu na kuchukua udhibiti wa chombo.

Kikosi hicho kiliongeza kuwa maafisa wa ngazi ya juu wa meli walihojiwa kwa onyo.

Serikali ya Gibraltar ilisema kuwa ina ushahidi ambao unakinzana na kauli zilizotolewa na nahodha na kwamba watatoa kauli yao hivi karibuni.

Imesema kuwa ina sababu ya kuamini kuwa meli ilikuwa imebeba mafuta ghafi kuelekea kituo cha Baniyas cha kusafisha mafuta nchini Syria, jambo ambalo Muungano wa Ulaya unasema ni kutoa usaidizi wa kifedha kwa serikali ya Syria.

Image caption MOD

Kukamatwa kwa meli hiyo ya mafuta kuliibua mzozo wa kidiplomasia baina ya Uingereza na Iran ambao umeongezeka katika kipindi cha wiki nne zilizopita.

Julai 19 meli ya mafuta iliyokuwa na bendera ya Uingereza Stena Impero ilikamatwa na vikosi vya ulinzi vya Iran katika njia muhimu ya meli za mizigo ilipokuwa ikielekea Hormuz.

Tehran ilisema kuwa meli hiyo vessel ilikuwa "inakiuka sheria za kimataifa za safari za majini " lakini Uingereza ililaani tukio hilo ililolitaja kama mfano wa "hali ya uharamia''.

Kwa pamoja mawaziri wa Mambo ya kigeni wa Uingereza Dominic Raab na balozi wa Iran nchini Uingereza wameamua kuachamajibijzano kuhusu kukamatwa kwa meli.

Bwana Raab alisema : "Hii si aina ya biashara . Hii ni kuhusu sheria ya kimataifa na kutekelezwa kwa mfumo wa sheria za kimataifa."

Balozi wa Iran Hamid Baedinejad alituma ujumbe wake wa Twitter akisema "haiwezekani kuendelea na biashara yaya mabishano ". Kituo cha kusafisha mafuta nchini Syria kiliwekewa vikwazo na Muungano wa Ulaya tangu 2014.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii