Wanawake walio na kisukari waweza kupata watoto njiti, utafiti wabaini

Mwanamke mjamzito akigusa na kuangalia tumbo lake la ujauzito Haki miliki ya picha Getty Creative

Wanawake wenye ugonjwa wa kisukari wana uwezekano mara nne wa kujifungua watoto njiti na hivyo kutoweza kuishi kuliko wasio na ugonjwa huo , umebaini utafiti

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Glasgow waliangalia rekodi za karibu wanawake 4,000 wa Uskochi wenye ugonjwa wa kisukari.

Walibaini kuwa viwango vya juu vya sukari mwilini miongoni mwa wanawake wajawazito wenye maradhi ya kisukari walikuwa na "uwezekano wa hatari " ya kupata watoto njiti.

Kiwango cha unene wa mwili (BMI) cha mwanamke mwenye ugonjwa wa kisukari pia ni sababu kubwa, utafiti ulibaini.

Watafiti pia walibaini kuwa theluthi tatu ya watoto wa aina hiyo wanaozaliwa kwa wanawake wenye ugonjwa wa kisukari hutokea wanapomaliza muhula kamili.

Kujifungua mapema

Dr Sharon Mackin, ambaye alifanya utafiti huo, amesema kuwa: "Ni muhimu kwamba sisi kama wataalamu wa huduma ya afya , tutafute njia bora za kuwasaidia wanawake wakati wanapokuwa na umri wa kupata ujauzito kudhibiti uzito wao na viwango vya sukari mwilini, ili wanapokuwa wajawazito iwe kwa kupanga au kwa kutopanga , wawe wamejiandaa na kupunguza hatari za matokeo mabaya.

"Ni muhimu kwa wanawake wenye kisukari wawe watu wenye kujali hili, na wawe na uwezo wa kupata ushauri nasaha wa awali kabla ya kupata ujauzito, hata kama ikiwezekana wapange ujauzito.

"Wanawake wenye ugonjwa kisukari pia wanapaswa kuwasiliana na kliniki zao za kisukari mapema iwezekanavyo mara wanapotambua kuwa ni wajawazito ili tuweze kuwaona na kuwasaidia mapema ."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uvumbuzi ambao "haukutarajiwa " wa utafiti ulikuwa ni kwamba watoto njiti walikuwa ni kiume zaidi kuliko wa kike miongoni mwa wanawake wenye aina ya 2 ya kisukari

Utafiti ulibaini kuwa kujifungua mapema kunaweza kuangaliwa kama "chaguo linalowavutia wengi " lakini kwamba utafiti zaidi unahitajika kabla ya kuidhinisha hilo kwa kuwa muda wa kujifungua mapema unatakiwa kupangwa.

Dr Mackin amesema kuwa swali la kujiuliza "linapaswa kuwa ni ikiwa kujifungua mapema kwa wanawake wote wajawazito wenye ugonjwa wa kisukari kunaweza kuwazuwia kujifungua watoto njiti ".

Amesema: "hatufahamu jibu kuhusu hili . Muda sahihi wa kujifungua wa nujauzito wa aina hiyo haujulikani."

Utafiti ulibaini kuwa watoto wachanga 5,392 walizaliwa kwa akina mama 3,847 wenye kisukari katika Uskochi mwenzi Aprili 1998 hadi Juni 2016.

Akina mama wenye aina ya 1 ya kisukari walikuwa na uwezekano mara tatu wa kupata watoto njiti, huku wale wenye aina ya 2 walikuwa na uwezekano wa kuwapata watoto hao mara nne

Viwango vya watoto njiti vilikuwa ni watoto 16.1 kati ya wazazi 1,000 miongoni mwa wanawake wenye aina ya 1 ya ugonjwa wa kisukari na watoto 22.9 kwa wanawake 1,000 miongoni mwa wanawake wenye aina ya 2 ya ugonjwa huo ililinganishwa na 4.9 kwa wanawake 1,000 miongoni mwa wanawake wote kwa ujumla.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Utafiti umebaini kuwa "kwa ujumla juhudi za kuboresha viwango vya sukari mwilini kabla na wakati wa ujauzito ni suala muhimu

Wanawake wenye aina ya 1 ya ugonjwa wa kisukari waliokuwa na uzazi wa watoto njiti walikuwa na kiwango cha juu ya wastani wa sukari katika damu yao kwa kipindi chote cha ujauzito wao, huku viwango vya kabla ya ujauzito vikiwa muhimu sana katika ubashiri wa uzazi wa watoto njiti miongoni mwa wale waliokuwa na aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari.

Watoto wachanga wenye uzito wa juu au wa chini walikuwa na uwezekano zaidi wa hatari ,ulibaini utafiti uliochapishwa na jarida maalumu linaloandika kuhusu ugonjwa wa kisukari- Diabetologia journal.

Dr Emily Burns, mkuu wa mawasiliano ya utafiti katika kituo cha utafiti wa ugonjwa wa kisukari nchini Uingereza -Diabetes UK, amesema : "Wanaweki wengi wenye ugonjwa wa kisukari wana ujauzito wenye afya na watoto wachanga wenye afya, lakini utafiti huu unahimiza umuhimu wa kuwasaidia wanawake kudhibiti viwango vyao vya sukari katika damu zao pale wanapopanga kupata ujauzito, ili kupunguza hatari ya matatizo kadri wawezavyo.

"Utafiti huo pia umeonyesha kuwa kupunguza uzito wa ziada, kwa wanawake wenye aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari ambao wana uzito wa mwili kupita kiasi, wanaweza kusaidia kupunguza hatari pia

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Umuhimu wa maziwa ya mama: Wanawake wachangia akiba ya maziwa kuokoa vichanga Kenya

"Tunahitaji utafiti kubaini njia bora zaidi za kubashiri ni nani yuko katika hatari ya kupata matatizo wakati wa ujauzito, kuhakikisha usaidizi unatolewa kwa wale wanaouhitaji zaidi''.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii