Mzozo wa Ebola: Kisa cha pili chathibitishwa kwenye mji wa mpakani mwa Kongo wa Goma

A health worker inoculates a child in Goma Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafis wa afya wamekuwa wakitoa chanjo ya Ebola mjini Goma

kisa cha pili cha ugonjwa wa Ebola kimebainika katika mji wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo unaopakana na Rwanda, kikiibua hofu ya kuwa ugonjwa huo unaoua unaweza kusambaa.

kisa hicho kilithibitishwa katika mji wa Goma, unaokaliwa na watu milioni mbili, maafisa wanasema.

Zaidi ya watu 1,600 wamekwisha kufa kutokana na Ebola katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo tangu mlipuko wa ugonjwa huo ulipotokea Agosti 2018.

Shirika la Afya duniani wiki iliyopita lilitangaza mlipuko wa ugonjwa huo kama dharura ya dunia ya afya.

Ni kiwango cha juu cha sauti ya dharura ambacho WHO linaweza kuitoa na imewahi kutolewa mara nne tu awali - ukiwemo mlipuko wa Ebola uliowakumba watu wa Afrika Magharibi kuanzia mwaka 2014 hadi 2016, ambao uliwauwa zaidi ya watu 11,000.

Hali ikoje katika mji wa Goma?

Ebola inaathiri majimbo mawili ya Kongo - kivu Kaskazini na Ituri. Goma ni mji mkuu wa jimbo la kivu Kaskazini na Unapatikana katibu tu na mji wa mpakani wa taifa jirani la Rwanda wa Gisenyi.

Kasisi mjini Goma alikufa kutokana na ugonjwa wa Ebola mapema mwezi huu .

Jumanne , Dr Aruna Abedi - ambaye anaratibu shughuli za huduma za uhgonjwa huo katika jimbo la Kivu Kaskazini aliliambia shirika la habari la AFP kuwa amefahamishwa kuhusu kisa cha pili cha Ebola.

"Hatua zote zimechukuliwa ili mgonjwa aliyepatikana ahudumiwa mjini Goma," imesema taarifa rasmi.

Image caption Ramani inayoonyesha mataifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Goma, na Rwanda

Eneo hilo linakaliwa na idadi kubwa ya watu na kuna hofu kuwa hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huo hadi ndani ya Rwanda.

Ingawa katika nchi hiyo hakuna kisa cha Ebola kilichokwisha thibitishwa , tayari nchi hiyo imekwishajiandaa kwa kuweka vituo vya matibabu ya Ebola na inaandaa vituo vitatu vya kuwatenga watu watakaopatikana na maradhi hayo hatari pindu kisa chochote kitakapojitokeza.

''Rwanda imefanya juhudi kubwa za kuwekeza katika maandalizi ya Ebola'' Alisema mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhamon Ghebreyesus wiki iliyopita.

"Lakini kama mlipuko wa Ebola unaendelea katika jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kuna hatari kubwa halisi ya kuenea katika nchi jirani."

Hali ni mbaya kw kiasi gani katika DR Congo?

Zaoidi ya watu 2,500 wamekwisha athiriwa na theruthi mbili yao walikufa kwa Ebola

Ilichua siku 224 kwa idadi ya visa vay Ebola kufika 1,000, lakini kwa kipindi cha siku 71 vilifikia watu 2,000.

Takriban visa 12 vinaripotiwa kila siku.

Hakuna chanjo?

Ndio.

Ina uwezo wa 99% na zaidi ya watu 161,000 wamekuwa wakichanjwa.

hata hivyo , sio kila mtu anayepokea chanjo- ni wale tu amnbao wamegusana moja kwa moja na wagonjwa wa Ebola , na wale waliokaribiana nao.

Chanjo hiyo ilitengenezwa wakati mlipuko wa ugonjwa huo ulipoibuka Afrika Magharibi na imekuwepo wakati wote wa mlipuko wa hivi karibuni.

Ni kwanini bado mlipuko haujadhibitiwa ?

Kukabiliana na maradhi hayo kumetatizwa na mzozo katika kanda hiyo.

Tangu mwezi January, kumekuwa na mashambulio 198 dhidi ya wahudumu wa afya au vituo vya matibabuna kusababisha kuuawa kwa watu saba na wengine 58 walijeruhiwa.

Tatizo jingine kubwa ni kuvamiwa kwa wahudumu wa afya kulikosababisha theluthi moja ya vifo katika jamii katika kituo maalumu cha matibabu ya Ebola

Inamaanisha kuwa watu ambao hawaji kutafuta matibabu na wanaweza kusambaza ugonjwa kwa majirani na ndugu zao.

Imekuwa ni vigumu kufahamu kiwango cha usambaaji wa virusi vya Ebola.

Je inafanya juhusi za kutosha kusaidia ?

Shirika la Afya duniani -WHO limekuwa wazi kwa miezi kadhaa kwamba halina pesa za kutosha za kukabiliana na tatizo la mlipuko wa Ebola.

Lilikuwa limekadiria kuwa linahitaji dola milioni 98 kukabiliana na mlipuko huo kati ya Februari na Julai. Lakini bado likakabiliwa na upungufu wa dola milioni 54.

Wbola ni nini ?

Haki miliki ya picha BSIP/Getty Images
  • Ebola ni kirusi ambacho mwanzo husababisha joto la mwili na kudhoofisha misuli na uvimbo kooni
  • Kisha mgojwa huanza kutapika, kuendesha na kuvuja damu ndani na hata nje ya mwili
  • Watu huambukizwa wanapogusana moja kwa moja kupitia michubuko ya mwili, au mdomo na pua, huku damu, matapishi, kinyesi au kugusa majimaji ya mwili ya mgonjwawa Ebola
  • Wagonjwa huwa wanakufa kutokana na ukosefu wa maji mwilini na kuharibikwa kwa viungo vya ndani vya mwili .

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii