Mbunge wa Kenya arejea India kulipa deni alilokopeshwa miaka 30 iliyopita

Richard Tongi na Kashinath Gawali Haki miliki ya picha RICHARD TONGI / RAVIKANT GAVLI
Image caption Richard Tongi na Kashinath Gawali

Kashinath Gavali, 75, makaazi wa Wankhedenagar katika mji wa Aurangabad nchini India alipata umaarufu miongoni mwa wanafunzi kutokana na biashara yake ambayo ilikuwa mkombozi kwa baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakiishi karibu.

Richard Nyagka Tongi alikuwa mmoja wa wanafunzi kama hao.

Richard, ambaye ni mbunge wa Kenya alisomea Aurangabad mwaka 1985 na alikuwa akiishi katika nyumba ya kukodisha karibu na duka la Gavali.

Mara nyingi hakupokea pesa alizotumiwa na familia yake kutyoka Kenya kwa muda aliyotarajia. Kutokana na hilo wakati mwingine alilazimika kukopa vitu vya matumizi kutoka kwa duka la Gavali.

Kashinath Gavali pia alimkopesha Richard na vitu kama maziwa, mkate, siagi na bidhaa zingine bila hofu yoyote.

Richard alirejea Kenya mwaka 1989 baada ya kukamilisha masomo yake lakini kila akifanya hesabu ya vitu vyake vya matumizi alikuwa akilikumbuka deni la Rupee 200 la Gavali na muda wote amekuwa akitamani kulilipa.

Alipopata uongozi

Maisha yalibadilika na Richard sasa ni kiongozi baada ya kujiunga siasa za Kenya ambapo alichaguliwa kuwa mwakilishi katika bunge la nchi hiyo.

Hata baada ya hadhi yake kupanda katika jamii alikumbuka deni la Gavali.

Wakati mwingine angelimwambia mke wake, 'Nitakutana vipi na Mungu wangu kama siwezi kulipa deni.' Pia aliomba apate nafasi ya kurudi tena India.

Haki miliki ya picha RAVIKANT GAVALI
Image caption Richard Tongi na familia ya Kashinath Gawali

Kurejea India, baada ya miaka 30

Hatimae miaka 30 baadae, Richard alipata fursa hiyo.

Richard ambaye ni naibu mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na masuala ya kigeni katika bunge la Kenya hivi karibuni alizuru taifa hilo kama sehemu ya ujumbe wa Kenya.

Baada ya kukamililisha kazi yake rasmi mjini Delhi alitembelea eneo la Aurangabad siku ya Jumapili akiwqa ameandamana ma mke wake ambaye ni daktari kutafuta nyumba ya Bw Gavali katika mtaa wa Wankhedenagar.

Mtaa huo ulikuwa umebadilika kabisa na kile alichokumbuka kumhusu muhisani wake ni jina la- 'Gavali'.

Na jina lenyewe alilitamka visivyo 'Gavaya', badala ya 'Gavali' kwa hivyo watu hawakufahamu anamtafuta nani haswa.

Lakini alipoelezea jinsi Gavali alivyopenda kuvaa vazi la fulana iliyofahamika kama 'banyan' kila mmoja alimtambua.

Kwa bahati nzuri mmoja wa watu Richard aliyekuwa akisoma nao alikuwa Kashinath binamu wa Gavali, na alikubali kumpeleka hadi nyumbani kwake.

Haki miliki ya picha RAVIKANT GAVALI

Jumapili moja kama mwendo wa saa moja jioni, Kashinatha alirejea nyumbani kujiandaa kwa chakula cha jioni kama ada yake, mwanawe wa kiume Nandkumar alimuita na kumfahamisha kuna mtu anaomba kukutana nae.

Lakini, Kashinath aliamua kukutana na wageni hao baada ya kula, kwa hiyo alishuka chini dukani baada ya kama dakika 15-20.

Alipofika alimuona mtu raia wa Kigeni wa mri wa makamo akimsubiri katika duka lake.

Mtu huyo alikuwa ameandamana na mwanamka na Kashinath alishangaa na kujiuliza ni kina nani.

Wote wawili walianza kububujikwa na machozi walipomuona Kashinath na kwa karibu dakika saba hawakuweza kusema lolote bali walilia kila walipomuangalia Bw. Gavali.

Gavali hakuweza kumkumbuka mtu huyo na alionekana kuchanganyikiwa japo tukio hilo lilimgusa sana

Na mtu huyo wa umri wa makamo aliyejitambulisha kama, Kashinath Gavali alikumbuka kila kitu.

Haki miliki ya picha RAVIKANT GAVALI

Richard na Kashinath walifurahi kukutana tena baada ya miaka mingi.

Wawili hao walijumuika pamoja kwa karibu saa tatu na katikati mazungumzo yao Richard alimfahamisha Kashinath kuwa anadeni lake la Rupee. 200.

Kisha akamkabidhi euro 250, Lakini Kashinath alikataa kuzipokea pesa hizo na kuongeza kuwa amefurahishwa sana na hatua ya Richard kumtembelea. Lakini, Richard alimsisitizia kuzipokea .

Richard alisema, "Ulinisaidia nikiwa katika hali ngumu zama hizo. Siwezi kusahau wema wako. Mimi ni mwana wa mkulima. Siwezi kuishi bila kulipa deni la mtu. Natawezaje kukutana na Mola wangu kama sitaweza kulipa deni lako?"

Kashinath alibubujikwa na machozi aliposikia manenoi hayo. Na baadae kupokea pesa hizo. Richard hatimae aliialika familia ya Kashinath Kenya na kuondoka.

Kashinath aliwasaidia wanafunzi wengi

Kashinath amewasaidia wanafunzi wengi kutoka familia masikini ambao walilipa madeni yao walipopata pesa kutoka kwa familia zao nje ya nchi.

Kutokana na uhusiano wa karibu aliojenga na wanafunzi hao baadhi yao humtembelea hadi wa leo.

Kashinath Gavali anasema, "hawa wanafunzi wote wanatoka mbali. Nawasaidia kwasababu naelewa hali ngumu wanazopitia.Tulikuwa masikini lakini tuliamua kuwasidia watu wengine wasiojiweza katika jamii kwa njia yoyote kadri ya uwezo wetu."

Anasema, "utamaduni wetu unatuambia kuwa mgeni ni ''Mungu''. Nimefuata muongozo huo maishani kwa kuwasaidia wanafunzi kwa vyovyote ninavyoweza. Pia tumeendelea kwa sababu ya wanafunzi hawa. Tumejenga nyumba yetu. Tumeanzisha biashara ya hoteli. Tumepata mafanikio haya kutokana na baraka za wananfunzi hawa kwa ukarimu wetu."

Hadithi hiyo ilianza mwaka 1985 ambapo ukoloni mpya ulijenga nyumba mpya katika mtaa wa Wankhedenagar karibu na Tasisi ya Maulana Azad mjini Aurangabad.

Nyumba hizo zilikabidhiwa wenyeji lakini baadhi yao walizikodisha kwa wanafunzi wa vyuo kutoka maeneo jirani wengi wao wanafunzi wa kigeni.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii