Kunyonyesha ni jambo muhimu katika ukuaji wa mtoto

Mama wawili wakizungumza huku wakinyonyesha watoto wao

Chanzo cha picha, Getty Images

Nilikwenda kwenye madarasa ya uzazi, ninunua sidiria za kuvaa wakati wa kunyonyesha- Nilikuwa tayari kabisa kuwa mama mnyonyeshaji.

Lakini siku mbili baada ya mtoto wangu kuzaliwa, maziwa yalikuwa yakitoka kidogo kidogo. Nilijaribu kuyakanda, nilikula vyakula vya mafuta, nilikunywa maziwa ya ng'ombe magaloni kwa magaloni. Lakini siku ya tatu, mkunga alinishauri nirudi hospitali: mtoto wetu alikuwa na njaa.

Ni ngumu

Chanzo cha picha, Getty Images

Niliposhauriwa kuanza kutumia pampu ya maziwa hospitalini, damu ilitoka badala ya maziwa.

''Nina matatizo gani? Mwili wangu unakataa hali ya kuwa mama?'' nikajiuliza. Mtoto wangu alikuwa akinyonya maziwa kwa nguvu ili aweze kupata maziwa kiasi chuchu zangu zilipata vidonda.

Laiti ningejua kuwa suala la kunyonyesha haliji tu lenyewe. ni mchakato wa kupanda na kushuka. Unaweza kufanikiwa kwa kujaribu mara kwa mara, kwa kuwa si rahisi mara zote, ni mchakato ambao unaweza kuumiza.

Ni upweke

Chanzo cha picha, Getty Images

Baada ya kufanikiwa mtoto wangu alianza kupata maziwa, nilikuwa na muda mfupi sana wa kulala, kuoga hata muda wa kujitazama kwenye kioo. Kutoka halikua jambo jema kwangu: ''Nilifikiri majirani wataonaje? maarafiki watafikiri nini?''

Maeneo niliyopenda kuyatembelea sikwenda tena kwa kuwa sikuwa nikipendelea kunyonyesha hadharani. Nilikuwa nikiamka usiku wa manane, pekeyangu na mtoto, nikijisikia mpweke nje ya ulimwengu, nilikuwa na msongo sikuwa na mtu wa kunisaidia.

Bora ningejua kuwa kujitunza mwenyewe ni muhimu pia kama ilivyo kwa kumtunza mtoto. Mama mwenye afya njema na aliyepata muda wa kupumzika ni bora zaidi kuliko aliye na wasiwasi mwingi na mwenye sonona

Chanzo cha picha, Getty Images

Mtoto wangu kwanza walimpatia maziwa ya unga hospitali, alilala kwa saa kadhaa. Nakumbuka niliwahi kuwaza mwenyewe kuwa kama nitahitaji kulala, nitaweza kumpa maziwa ya kopo badala ya kumnyonyesha.

Haikunichukua muda kuanza kujiona mwenye hatia. Maziwa ya kopo yakaanza kuacha mabaki kama utando kwenye ulimi- ilikuwa na harufu mbaya na yakaonekana hayana uhalisia. Ilikuwa kama nilikuwa namlisha mtoto wangu vyakula visivyo na faida kwenye mwili wake.

Kila wakati nilikuwa nikijiambia kuwa : ''Ningejaribu zaidi.Kwa kweli sikuwa nahitaji muda zaidi wa kulala.''

Laiti ningejua kuwa hali ya kujisikia mwenye hatia haiishi. Lakini ni jambo ambalo halina utetezi, kila mtu atafanya kile ambacho anaona kinamfaa- kunyonyesha au la.

Pata msaada

Chanzo cha picha, Getty Images

Unyonyeshaji ni suala la gharama kubwa, kwa kila changamoto, kuna gharama ya fedha kwa kila ufumbuzi wenye kuleta nafuu.

Niligundua kwenye duka nililokuwa nimeenda kutafuta tiba nikaziona za kila namna.

Lakini tiba muhimu kwangu ilikuwa ni kwenda kwenye madarasa yanayotoa elimu kuhusu unyonyeshaji na kupata msaada kutoka kwa wataalamu na watu wenye uzoefu.

Laiti ningalijua kuwa sikuwa peke yangu, nami ni miongoni mwa watu wengi wanaopata shida kwenye suala la kunyonyesha. Kuna msaada unaopatikana, na kuomba msaada ni jambo zuri zaidi unaloweza kufanya.

Chanzo cha picha, Getty Images

Unyonyeshaji ni kuchagua. Nafikiri uwe ni uchaguzi wa mtu mwenyewe, lakini kushindwa au kutotaka kunyonyesha hakukufanyi kuwa mama mbaya.