I Am Hannah: Igizo ambalo Gemma Chan anaeleza tatizo hilo kwa wanawake

Gemma Chan kwenye filamu I Am Hannah Haki miliki ya picha Channel 4

Shinikizo la kuwa na watoto huweza kutoka kila mahali.

Mzazi ambaye ana shauku ya kuwa na wajukuu. Marafiki ambao hivi karibuni wamepata watoto. Wapenzi ambao hukutana kwa mara ya kwanza na kuulizana kuhusu mipango ya baadae.

Lakini pia shinikizo kubwa zaidi vijana hujiwekea wenyewe.

Suala la kutokuwa na mtoto katika umri wa miaka ya 30 lilionekana kwenye igizo la channel 4 liitwalo I Am Hannah, nyota Gemma Chan. Ni moja kati ya filamu za Televisheni ambayo inalenga simulizi za wanawake.

Katika I Am Hannah, Chan mwenye miaka 36, amecheza kama mwanamke ambaye amekuwa akizusha maswali mengi kama ana mipango ya kuwa na familia.

Ujumbe wa mchezo huu ni kuwafanya watazamaji kutazama mazingira yao na mashinikizo wanayokutana nayo.

Haki miliki ya picha Getty Images

Chan anaeleza: ''masuala yanayojitokeza kwenye mchezo huu yanakuja kutoka kwenye mazungumzo ambayo nimekuwa nayo na marafiki zangu, mama yangu, dada yangu.

''Nina marafiki ambao wamekuwa kwenye shinikizo la namna hiyo hiyo anayopitia Hannah. Siwezi sema nilichopitia ndicho alichopitia, kuna tofauti nyingi.

Hannah ameonekana akikutana na wanawake kadhaa kupitia Apps za wapenzi kila mmoja na vipaumbele vyake na maoni kuhusu watoto. Alikuwa akijadili kuhusu kugandisha mayai. Na anakabiliwa na shinikizo kwa mama yake kuhusu kwa nini hayuko tayari kuanzisha familia. ''Siku moja utaamka ukiwa na miaka 40,'' humwambia.

''Uhusiano wa mama na binti ni wa kipekee wenye mapenzi tele lakini kunakuwa na mashinikizo hasa mzazi anapotaka mtoto wake awe na mafanikio kwenye jambo fulani,'' Chan anasema. ''Nafikiria mashinikizo kwa Hannah yanatoka nje, lakini pia yapo matarajio ya ndani ambayo Hannah anajielekezea mwenyewe.

Alazimishwa kuchagua kati ya mwanawe na familia yake

"Nina miaka 38 na watoto 35''

Mwanzoni mwa mwaka huu, mtaalamu wa saikolojia ya tabia Paul Dolan alianzisha mjadala mkali alipotoa maoni kuwa watu mara nyingi huwa na furaha wasipokuwa na watoto wala mke au mume.

''Labda tunawaona watu wasio na wapenzi kama tishio , au labda tunawaonea wivu kwa kuwa tunawaona wamekuwa huru, au hatuwezi kujizuia kufanya ulinganisho na mauisha yetu tunaposikia namna wengine walivyo na furaha.'' Alisema Paul Dolan.

Haki miliki ya picha Channel 4

Je, watu wanapaswa kufikiria namna yakuuliza wanapotaka kufahamu ikiwa vijana wana mipango ya kuwa na watoto?

''Labda kwa kuwa huenda ni eneo la faragha kwa baadhi ya wanawake ameeleza Lashchyk. ''Hata hivyo nafikiri kama mwanamke ameamua kutokuwa na watoto basi ataweza kujiamini na kuyapuuza maoni ya watu kuhusu msimamo wake.

''Mimi binafsi sikasirishwi na hilo, na ninaelewa kuwa watu mara nyingi hutoa maoni bila kufikiri, hii inaonyesha mtu kutoweza kufikiria maisha tofauti na wanayoyaishi''.

Haki miliki ya picha Getty Images